Chuo Kikuu cha Rwanda (UR) kimerejesha programu zake za shahada ya kwanza ya miaka minne, na kurejea katika muundo wa hapo awali.
Kwa miaka mitano ilikuwa inajaribu mfumo wa kutoa shahada baada ya miaka mitatu.
Chuo hicho ni Chuo cha Umma chenye wanafunzi zaidi ya 30,000 waliosambazwa katika vyuo saba na 'campus' tisa.
Katika mwaka wa masomo wa 2017, sayansi ya kijamii na programu tofauti za sayansi zilipunguzwa hadi muda wa miaka mitatu badala ya miaka minne ya hapo awali.
Maafisa walieleza kuwa uamuzi huo ulifanywa baada ya kubaini kuwa kozi za sayansi kama vile usanifu, uhandisi na dawa ndizo zinazopaswa kuendelea zaidi ya miaka mitatu.
"Wahitimu na waajiri walituambia mara kwa mara kuwa mtaala uliobanwa wa miaka mitatu uliwaacha wanafunzi wakikosa maarifa na ujuzi muhimu. Tulijaribu kuweka mfumo wetu uwe kama vyuo vikuu vya kikanda vinavyotoa programu za miaka mitatu, lakini tathmini yetu ilionyesha kuwa mbinu hii haikuwa inatoa matokeo yaliyotarajiwa,” alisema Didas Muganga Kayihura, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Rwanda.
Uamuzi wa kufanya shahada ya kwanza kwa miaka mitatu hapo awali ulikuwa unafuata mifumo katika nchi jirani kama vile Uganda na Kenya, ambapo vyuo vikuu vilifupisha kw miaka mitatu.
Nchini Rwanda, hatua hii ilizua mjadala iwapo mfumo kama huo unaweza kutoa wahitimu ambao wanakidhi viwango vya kitaaluma.