Chama kimoja cha upinzani nchini Kenya kimeweka pingamizi mahakamani kupinga hatua ya kutuma walinda amani katika kisiwa hicho cha Caribbean./Picha: Reuters  

Jeshi la polisi nchini Kenya kimeazimia kutuma walinda amani nchini Haiti, ndani ya wiki chache zijazo licha la pingamizi la Mahakama, Rais wa nchi hiyo William Ruto amesema.

"Huenda watu wa Haiti bado wanatusibiri, kwa neema za Mungu, bila shaka inaweza kuwa ndani ya wiki zijazo, tutatuma polisi wetu kulinda amani," alisema Ruto wakati wa risala yake aliyoitoa katika eneo la kati la Kenya siku ya Jumapili.

Kenya imeazimia kuongoza shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa kusaidia kurudisha amani katika nchini hiyo iliyokumbwa na vurugu kubwa.

Nchi hiyo ya Afrika Mashariki inalenga kutuma maofisa 1,000 katika operesheni hiyo maalumu.

Mchakato wakabiliwa na upinzani

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliridhia mchakato huo Oktoba mwaka jana, licha ya pingamizi kutoka Mahakama ya Kenya mwezi Januari mwaka huu.

Katika maamuzi yake, Mahakama hiyo ilisema kuwa serikali haikuwa na mamlaka ya kutuma polisi hao nje ya nchi bila makubaliano ya awali.

Serikali ilipata makubaliano hayo mnamo Machi 1 na Ruto aliambia BBC mwezi uliopita kwamba alitarajia jeshi la Kenya kwenda Haiti ndani ya wiki.

Lakini chama kimoja cha upinzani nchini Kenya kiliwasilisha kesi mpya kujaribu kuizuia. Mahakama kuu ya Kenya inatazamiwa kuangazia kesi hiyo Juni 12.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu pia yameshutumu polisi wa Kenya kwa kutumia nguvu kupita kiasi na kutekeleza mauaji kinyume cha sheria.

TRT Afrika