Mkutano kati ya Rais William Ruto na Mkuu wa Mahakama, Jaji Mkuu Martha Koome ulifanyika kufuatia mvutano wa muda kati yao.
Mkutano huo ulihudhuriwa na maspika wa bunge pia.
Rais Ruto amekuwa akikashifu mahakama kwa kile alichoita nia ya kuharibu mipango yake ya miradi ya maendeleo.
Ruto pia alitoa shutuma kuwa kuna majaji amabo ni wafisadi, Kwa upande wake makahama ilisema kuwa matamashi hayo ni sawa na rais Ruto kutaka kuwa dikteta ilhali katika katiba ya Kenya mahakam ima uhuru wake.
"Mkutano umefanyika kufuatia ombi kutoka kwa mahakama"
"Mkutano umefanyika kufuatia ombi kutoka kwa mahakama," taarifa kutoka Ikulu ya Kenya imesema.
Katika maazimio ya mkutano huo ni pamoja na kukubaliana kuwa ufisadi bado ni changamoto kubwa kwa taifa na tayari imeota mizizi katika vitengo vya serikali , bunge na mahakama. Na kwamba inasababisha mipango ya maendeleo kuwa ngumu.
Ikikumbana na ufisadi mkutano huo umekubaliana pia na maswala matatu:
- Kuhakikisha majaji 25 wengine waandikwe katika mahakama kuu
- Kuhakikisha majaji 11 wanapewa ajira katika mahakama ya rufaa.
- Kuwezesha mpango wa kukodisha gari ili kuwezesha usafiri wa maafisa wa mahakama
Vitengo vitatu vya seriklai vimekubaliana kutengeneza sera zao binafsi na mwongozo wa kisheria ili kukumbana na ufisadi.