Ikulu ya Kenya imetangaza kuwa majadiliano hayo yenye mada ya " let's engage" ina nia ya rais kusikiliza matakwa ya wananchi/ Picha Rais William Ruto

Rais William Ruto atafanya majadiliano kupitia mtandao wa X Spaces na wananchi kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na moja jioni.

Ikulu ya Kenya imetangaza kuwa majadiliano hayo yenye mada ya " let's engage" ina nia ya rais kusikiliza matakwa ya wananchi hasa Gen Z ambao wamekuwa wakifanya maandamano kwa wiki tatu tangu 18 Juni 2024.

Mtandao wa X umekuwa chombo muhimu kwa vijana nchini humo kupanga maandamano ya amani na hata mada za kampoeni dhidi ya serikali ya Rais Ruto.

Tarehe 19 Juni, 2024 siku moja baada ya maandamano ya mitaani kuanza, vijana walifanya majadiliano kupitia mtandao wa X ambao ulivutia zaidi ya washiriki 470,000. Hii ni kati ya idadi kubwa kuwahi kushuhudiwa katika mtandao huo.

Maoni ya wananchi

Wananchi wamekuwa na maoni tofauti baada ya rais kutangaza kuwa atajitokeza kujadiliana nao moja kwa moja mtandaoni.

@_PalM3r amemjibu rais akidai "Sisi sio wenyeji wa majadiliano hayo, Rais anafaa kuwa mgeni kwa majadiliano, hivyo tu."

@darrenvickmell3 amesema, "tunataka kuongoza majadiliano, si wewe."

@Gideon_Kitheka naye amesema, "tuko tayari kuongea nawe rais."

Wengine tayari wametoa maoni ya mabadilko ambayo wanataka rais ayafanye.

"Tunaamini kwamba utaweka sheria zinazofaa kwa washiriki wote. Mheshimiwa Rais, tafadhali kumbuka kuweka kipaumbele cha kusikiliza na kuchukua kumbukumbu badala ya kuzungumza. Ni busara kwa njia hiyo kwako, kwa mkutano huu . Waache GenZ wazungumze sana," @TchaWicky_Tech amesema.

@bungomaduke amesema, "Asante rais kwa kukubali kutimiza ahadi ya kujadiliana nasi, tutakuwepo na kuongea nawe."

TRT Afrika