Wafungwa 37 wameachiliwa na Rais William Ruto  / Picha: getty

Rais William Ruto amewasamehe wafungwa 5000 ambao walikuwa wamehukumiwa vifungo tofauti.

Uamuzi huo umechapishwa na gazeti la serikali.

"Kwa kutumia mamlaka yaliyothibitishwa na katiba...na sheria ya nguvu ya rehema rais na kamanda mkuu wa vikosi vya ulinzi vya jamhuri ya Kenya baada ya mapendekezo ya kamati ya ushauri kuhusu mamlaka ya rehema alikubali ombi "

Kati ya watu 37 waliopewa rehema baada ya kutoa ombi, ni mkurugenzi mkuu wa zamani wa Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya, KEMRI, Davy Kiprotich Koech.

Koech alipewa kifungo cha miaka sita Septemba 2021.

Alihukumiwa kwa kupata dola 135,772 kwa njia ya ufisadi.

Rais Ruto pia amewasamehea wafungwa 2,944 walioshitakiwa kwa uhalifu ndogo ndogo , na wakapewa kifungo cha miezi sita au chini. Wameachiliwa kwa kuonyesha tabia nzuri.

Wafungwa wengine 2,117 ambao walikuwa na kifungo kirefu na wamebakisha miezi sita au chini kumaliza kifungo chao , wameachiliwa huru.

Gazeti hilo la serikali imetangaza kuwa rais Ruto pia alibadilisha hukumu za kifo zilizotolewa kufikia tarehe 21 Novemba 2022 kuwa kifungo cha maisha.

TRT Afrika