Rwanda na Bahamas zimesaini makubaliano ya kuondoa viza kati yao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Olivier Nduhungirehe na mwenzake wa Bahama Frederick Mitchell walitia saini mkataba wa makubaliano kuhusu Msamaha wa Mahitaji ya Visa.
Nchi hizo mbili zimekubaliana kufungua njia kwa raia wao kusafiri kati yao bila masharti ya viza.
Makubaliano hayo yalitiwa saini Jumatatu, Septemba 23, mjini New York ambapo viongozi hao wanahudhuria Mkutano Mkuu wa 79 wa Umoja wa Mataifa.
"Hatua muhimu katika uhusiano wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Bahamas," Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda ilisema. Mkataba huo unatumika kwa wamiliki wote wa hati za kusafiria, kulingana na Wizara.
Wakati wa ziara yake katika Visiwa vya Carribean mnamo Julai 2023, Rais Paul Kagame alitembelea Bahamas wakati nchi hiyo ikiadhimisha miaka 50 ya uhuru kutoka kwa Uingereza.
Alikutana na Waziri Mkuu Philip Davis. Viongozi hao wawili pia walijadili njia za kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Kagame pia alitunukiwa 'Tuzo ya Ubora,' heshima kubwa zaidi kwa kutambua urafiki wake kwa serikali na watu wa Bahamas.
Rais kagame amekuwa mtetezi wa uhusiano wa karibu kati ya Afrika na nchi za Carribean.
Mwaka 2022 akiwa katika ziara yake ya Jamaica mwaka 2022 Paul Kagame alisema kuwa Caribbean na Afrika zina mambo mengi yanayofanana, kuanzia watu, akieleza kuwa ni uhusiano wa kina ambao umbali wa kijiografia hauwezi kuondoa.
"Lazima tushughulikie masuala ya visa na kuhakikisha tunaunda msamaha ili tuhimize uhusiano huu tukijua kwamba tuna nia ya mtu mwengine, tunaweza kufaidika," alisema.