Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis ameonya kuhusu athari za akili mnemba / Picha: AP

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis siku ya Alhamisi aliwataka viongozi wa kisiasa, kiuchumi na biashara katika Kongamano la Kiuchumi Duniani (WEF) mjini Davos, kuweka uangalizi wa karibu wa maendeleo ya akili mnemba, yaani AI, akionya kwamba teknolojia inaweza kuzidisha "mgogoro wa habari potofu" unaoendelea kukua.

Katika ujumbe uliosomwa katika mkutano wa kila mwaka katika mji huo wa Uswizi, ambao kwa sehemu unaangazia maendeleo ya akili mnemba mwaka huu, Papa alisifu uwezo wa teknolojia lakini akasema pia unazua wasiwasi kuhusu mustakabali wa binadamu.

"Matokeo ambayo A.I. inaweza kutoa hayawezi kutofautishwa na yale ya wanadamu, na hivyo kuzua maswali kuhusu athari yake katika kuongezeka kwa mgogoro katika jukwaa la umma," Papa Francis alisema.

"Ili kukabiliana na matatizo ya A.I., serikali na wafanyabiashara lazima wafanye bidii na umakini," alisema katika taarifa hiyo iliyosomwa kwa niaba yake katika mkutano wa Davos na Kadinali Peter Turkson, afisa wa Vatican.

Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki tangu 2013, ameangazia masuala ya maadili yanayozunguka akili bandia katika miaka ya hivi karibuni.

Alizungumza kuhusu teknolojia katika mkutano wa viongozi wa Kundi la Saba nchini Italia Juni 2024, na akasema watu hawapaswi kuruhusu algoriti kuamua hatima yao.

Papa pia alikuwa muathirika wa picha bandia mwanzoni mwa 2024, iliyotengezwa na programu ya kutengeneza picha, ambayo ilionekana kumuonyesha akiwa amevalia koti jeupe lenye urefu na shanga ya mguu.

TRT Afrika