Ombi limetolewa bungeni Kenya na Mutuse Eckomase Mwengi, mbunge wa eneo la Kibwezi magharibi kumuondoa madarakani Naibu Rais wa nchi hiyo Rigathi Gachagua.
Gachagua anashutumia kwa kukiuka katiba na sheria nyengine.
"Kwa tarehe tofauti, Mtukufu Rigathi Gachagua, ameendelea kutoa matamshi ya kuwabagua, kuwatenga na kuwanyima isivyo halali sehemu ya watu wa Kenya na mikoa ya Jamhuri ya Kenya fursa sawa kwa uteuzi wa watumishi wa umma na mgawanyo wa rasilimali za umma," Muswada huo unasema.
Malalamishi dhidi ya Naibu Rais
Muswada huo umeorodhesha masuala kadhaa dhidi yake ikiwemo:
Gachagua amenukuliwa akisema,
"Mimi nikasema hiyo haiwezekani. Nikasema yule mwenye hii ng’ombe na kuichunga na kuitunza, kwanza akamue maziwa, yeye na watoto wake wakunywe, ile itabaki aitie majirani. Hata yule alikuwa anapiga kelele akisema hii ng’ombe ni bure na haiwezekani kama kunayo imebaki pia apewe, kama hakuna imebaki atembee. Si hiyo namna hiyo?”
" Rais mnamjua, mimi mnanijua msimamo wangu, ya kwamba watoto wakiwa wengi, kuna wale kwanza wa kuangaliwa, si mnajua?"
“Na mimi mkaniambia nimsaidie Rais kwa kazi! Lakini nikiwa hapo kwa serikari, nikue pia nikichunga mambo ya watu wa Mlima! Niendelee kuchunga mambo ya Mulima, ama nisichunge?"
Kukiuka heshima kwa Rais
Muswada huo pia unadai kuwa Naibu Rais Gachagua hatatoa heshima ya kutoka kwa serikali na Baraza la Mawaziri kwa miaka miwili iliyopia.
Unatoa mfano wa mnamo au karibu 30 Aprili 2024, Baraza la Mawaziri lilifanya uamuzi wa uhamishaji wa watu wanaoishi kando ya Mto Nairobi.
Anashutumiwa kwa kutoa matamshi kinyume na uamuzi huu
Gachagua anashtumiwa kwa kutomheshimu Rais. Muswada huo umetoa mifano kadhaa:
Muswada huo unamkashifu Naibu Rais kwa kukiuka sheria ya uendeshaji wa serikali ya Kaunti ya Jiji la Nairobi. Anadaiwa kuwa katika mkutano wa hadhara aliwachochea wananchi dhidi ya maagizo halali ya jiji hilo.
Gachagua pia anatuhumiwa kwa kutoheshimu viongozi wa mahakama.
"Mwezi Machi 2023, Naibu Rais alitoa matamshi dhido ya Jaji Esther Maina na akitishia kuchukua hatua dhidi ya Jaji kwa ukiukaji mkubwa wa Katiba. Jaji huyo alikuwa ameamua kesi ambapo Gachagua alihusika na akaamuru ailipe serikali shilingi milioni 200 ( zaidi ya dola milioni 1.5) mapato ya rushwa.
Muswada unadai matamshi yake kwa Jaji huyo yanadhoofisha utendaji na uhuru wa majaji kutoa maamuzi.
Naibu Rais na Mali yake
Muswada unadai kuwa Naibu Rais amejipatia mali nyingi zaidi kuliko mapato yake.
Inadai kuwa kwa miaka miwili iliyopita, Gachagua amejipatia mali yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 5.2 ( zaidi ya dola milioni 40) ilhali mapato yake ya kila mwaka ni takriban shilingi milioni 12 ( zaidi ya dola 96,000).
Muswada unamshutumu kwa kupata mali hii kupitia mke wake, watoto wake na jamaa zake wengine.
Ukiukaji wa sheria zaidi
Muswada unamshutumu Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa kutoa matamashi yasiyo ya heshima kwa Mkuu wa Mamlaka ya Ujasusi.
" ...Wakurugenzi watatu walifukuzwa na kupangiwa kazi za madawati katika Wizara kote Serikalini. Wakurugenzi Wasaidizi 13, wanaume na wanawake walio na rekodi iliyothibitishwa waliondolewa kwenye Ujasusi wa Kitaifa Huduma, ikiacha ganda chini ya Mkurugenzi Mkuu ambaye hana uwezo wa kuendesha Shirika. Na hiyo ndiyo sekta ya usalama ilijipata katika hali ya tahadhari, hasira ya watu wa Kenya..." Gachagua ananukuliwa.
Muswada unadai zaidi kuwa "Mheshimiwa Rigathi Gachagua amepanga pamoja na makampuni katika sekta ya chai ili kuzuia Maendeleo ya Mamlaka ya Chai ya Kenya kutokana na kutekeleza mapato ya chini yaliyohakikishwa ambayo yangefanya kunufaisha wakulima wadogo wa chai.
Pili, anadaiwa kuwashawishi wanafamilia wake, washirika, washirika na wakala kuchukua udhibiti wa chama cha ushirika cha ndani (jina limehifadhiwa) ambayo wanavuja kifedha.
Licha ya tuhuma hizo, Naibu Rais amesema kuwa amejiandaa kwa uamuzi wowote utakaotolewa dhidi yake.
Haya na mengineyo yanamkumba huku Rais William Ruto akiwa kimya.