Takriban watu 30,000 wanaoshukiwa kuwa na maambukizi ya Mpox wameripotiwa barani Afrika kufikia sasa, wengi wao wakiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC , Shirika la Afya Ulimwenguni lilisema Jumatatu.
Zaidi ya watu 800 walikufa kwa magonjiwa yanayhusishwa na ugonjwa huo katika bara zima , shirika la WHO lilisema katika ripoti yake.
Nchi jirani ya Burundi pia imeripotiwa imekumbwa na mlipuko huku maambukizi yakiongezeka.
Mpox inaweza kuenea kupitia mawasiliano ya karibu.
Kwa kawaida husababisha dalili zinazofanana na mafua na vidonda vilivyojaa usaha mwilini.
Shirika la afya ya Umoja wa Afrika , Africa CDC lilisema maambukizi14,957 na vifo 739 viliripotiwa kutoka majimbo saba yaliyoathiriwa mnamo 2023.
Hii ni ongezeko ya 78.5% ya maambukizi mapya kutoka 2022.
Kulikuwa na takriban maambukizi 29,342 na vifo 812 kote barani Afrika kuanzia Januari hadi Septemba 15 mwaka huu, kulingana na ripoti ya WHO.
Jumla ya maambukizi 2,082 yaliyothibitishwa yaliripotiwa kote ulimwenguni mnamo Agosti pekee, idadi kubwa zaidi tangu Novemba 2022, WHO ilisema.
Siku ya Jumamosi, mfuko wa Benki ya Dunia wa janga la ugonjwa huo ulisema utatoa dola milioni 128.89 kwa nchi kumi za Afrika kusaidia kupambana na mlipuko huo.