Moussa Camara alikuwa rais wa Guinea kutoka 2008 hadi 2010 / Picha: AFP

Moussa 'Dadis' Camara mwenye umri wa miaka 59 ni afisa wa zamani wa jeshi la Guinea ambaye alikalia kiti cha urais wa nchi hiyo kupitia mapinduzi ya serikali mwaka 2008.

Aliongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuanzia tarehe 23 Desemba 2008 hadi 15 Januari 2010.

Alikuwa kiongozi wa Baraza la Kitaifa la Demokrasia na Maendeleo yaani National Council for Democracy and Development.

Kulingana na katiba ya Guinea , rais wa Bunge la Kitaifa alipaswa kushika urais wa Jamhuri katika tukio la nafasi iliyo wazi, na uchaguzi mpya wa urais ulipaswa kufanywa ndani ya siku 60.

Lakini Saa sita baada ya kifo cha Conté, kutangazwa taarifa ilisomwa kwenye televisheni ikitangaza mapinduzi ya kijeshi, yakiongozwa na Kapteni Camara.

Moussa Camara alilaumiwa kwa mauaji ya watu 157:  Picha AFP

Mnamo Septemba 28, 2009, wanachama wa chama cha upinzani waliandamana katika ukumbi wa michezo huko Conakry, wakitaka Camara ajiuzulu.

Walinzi wa rais "Red Berets", wakiongozwa na Abubakar "Toumba" Diakite, walihusika na vurugu hizo, kuwafyatulia risasi, kuwapiga visu, na kuwabaka raia waliokuwa wakitoroka na genge hilo liliwaua takriban watu 157.

Mnamo Desemba 3, 2009, Camara alipigwa risasi na kujeruhiwa kichwani na majeshi chini ya uongozi wa mlinzi wake , Abubakar "Toumba" Diakite.

Baada ya Kapteni huyo kuondoka Guinea, uchunguzi ulianzishwa kuhusu mauaji hayo yaliyofanyika kuanzia 2010 hadi 2017.

Mnamo Septemba 27, 2022, Moussa Dadis Camara alifungwa gerezani.  / Picha: Reuters

Mnamo 2018, kamati iliundwa kuandaa kesi hiyo, lakini wasiwasi uliibuka juu ya ukosefu wa maendeleo kwa sababu haikuwa ikikutana mara kwa mara.

Aliyekuwa mkuu wa kijeshi - Kanali Mamady Doumbouya - ambaye aliingia madarakani baada ya mapinduzi mnamo 2021, aliamuru kesi hiyo ifanyike.

Mnamo Septemba 27, 2022, Moussa Dadis Camara alifungwa gerezani.

Guinea inatawaliwa na kiongozi wa kijeshi Mamady Doumbouya, ambaye alichukua mamlaka katika mapinduzi mwaka 2021.

TRT Afrika