Vikosi vya Rapid Support Forces nchini Sudan ambavyo vimekuwa vikipambana na jeshi la Sudan kwa ajili ya kudhibiti nchi hiyo vimesema vimeteka eneo la Nyala, mji wa pili kwa ukubwa siku ya Alhamisi.
Kikundi hicho kimedai kimeteka makao makuu ya jeshi huko Nyala na kukamata vifaa vyake vyote.
Bado jeshi la Sudan halijatoa taarifa yoyote kuhusu madai hayo yaliyotolewa na kikundi hicho.
Kutekwa kwa mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini magharibi mwa nchi kunakuja wakati pande hizo mbili zikitarajiwa kufanya upya mazungumzo huko Jeddah.
Maongezi hayo yanaongozwa na Saudi Arabia, Umoja wa Afrika na Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali, IGAD.
IGAD ni muungano wa Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia, South Sudan, Sudan, na Uganda
"Mkurugenzi Mkuu wa IGAD Workeneh Gebeyu, tayari yuko Jeddah kwa niaba ya marais wa kanda ya IGAD," Nuur Mohamud Sheekh, msemaji wa IGAD ameiambia TRT Afrika.
" IGAD inajitolea kushiriki katika mazungumzo na mashauriano na wadau wote wa Sudan na inapanga kuitisha mchakato wa kisiasa unaojumuisha eneo la IGAD," Sheekh ameongezea.
Jeshi la Sudan halijatoa maoni yoyote kuhusu hali kujibu ombi la maoni, na kuzima kwa mtandao kulifanya iwe vigumu kuthibitisha madai hayo mara moja.
Wakati RSF imekita kambi katika sehemu kubwa ya mji mkuu Khartoum nchini Sudan, jeshi limeweza kulinda vituo vyake muhimu huko.
Wakati huo huo, sehemu kubwa ya serikali imehamia Bandari ya Sudan kwenye pwani ya Bahari Nyekundu.
Takwimu zaonyesha kuwa tangu vita kuanza nchini Sudan 15 Aprili, zaidi ya watu wameuawa 9,000 na wengine milioni 5.6 kuyahama makazi yao tangu Aprili.