Mauzo ya madini Rwanda yafika zaidi ya dola milioni 360

Mauzo ya madini Rwanda yafika zaidi ya dola milioni 360

Kati ya Aprili na Juni 2023, Rwanda imeuza zaidi ya kilo milioni 6 za madini
Ufuaji wa madini Randa unailetea nchi mapato makubwa  / Photo: Reuters

Rwanda inasema kuwa nchi imefanya mauzo mengi ya madini kati ya Aprili na Juni, ikilinganishwa na kati ya Januari na Mei mwaka huu .

Mapato kutokana na mauzo ya madini katika robo ya pili ya 2023 yalikuwa dola milioni 362, kutoka dola milioni 247 katika robo ya kwanza. Hii ni kulingana na ripoti ya Bodi ya Madini, Petroli na Gesi ya Rwanda (RMB).

Bodi hiyo inasema hali ikiendela hivi basi serikali itafikia lengo lake la mauzo ya mwaka 2024, ambayo ni $1.5 bilioni.

Je ni madini gani yalileta mapato makubwa?

Mauzo ya zaidi ya kilo milioni moja ya "cassiterite" yamemevutia mapato ya zaidi ya dola milioni 18. Cassiterite hutumika kwa utengenezaji wa bidhaa zinazotokana kama vile bati, vito, vifaa vya ujenzi na zaidi.

Kilo 4,696 za dhahabu zilileta dola milioni 302.6.

Kilo 587,015 ya Coltan ilileta zaidi ya dola milioni 27.8 . Colatan hutumika kuunda vifaa vya elektriniki kama kompyuta na simu za rununu.

Mauzo ya kilo 635, 435 ya Wolframite ilileta zaidi ya dola milioni 111. Madini aina ya wolframite hutumika kutengeneza nyuzi za umeme na pande za mashine tofauti.

Madini mengine yameletea nchi zaidi ya dola milioni 4.9.

TRT Afrika