Jiji la Kampala nchini Uganda. Picha TRT Afrika

Uganda imeongeza makadirio ya matumizi ya fedha za umma kwa mwaka wa fedha 2024/25 (Julai-Juni) kwa asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka uliopita, huku fedha nyingi zikielekezwa katika miundombinu ya uchukuzi, Wizara ya Fedha ilisema Alhamisi.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X, Wizara ya Fedha ilisema Waziri wa Fedha Henry Musasizi alituma pendekezo lake la bajeti bungeni.

Serikali itatumia jumla ya shilingi trilioni 58.3 za Uganda ($15.02 bilioni) mwaka 2024/25.

Vipaumbele katika mwaka ujao wa fedha, Wizara ilisema, vitajumuisha ujenzi wa barabara za kimkakati na reli ya kisasa (SGR) miongoni mwa zingine.

TRT Afrika