Istanbul iko tayari kuwapa taji wafalme wapya wa Barani Ulaya.
Jiji la kihistoria la Uturuki linaandaa mchuano wa Jumamosi wa Ligi ya Mabingwa kati ya wababe Manchester City na miamba wa Italia, Inter Milan.
Ni mara ya kwanza kwa vilabu hivi vya Uingereza na Italia kukutana katika fainali ya shindano kuu la kandanda la vilabu barani Ulaya.
Fainali ya Ligi ya Mabingwa inarejea katika Uwanja wa Olimpiki wa Ataturk, Istanbul, baada ya takriban miongo miwili. Uwanja huu unaweza kukaribisha mashabiki 72,000.
Mashabiki wangetamani kurudiwa kwa msisimko wa 2005 uliopewa jina la "Muujiza wa Istanbul," fainali ambayo pia ilishirikisha vilabu vya Uingereza na Italia.
Liverpool, wakiongozwa na Steven Gerrard, walipindua pungufu ya mabao matatu ya muda wa mapumziko ndani ya dakika sita pekee na kuipeleka AC Milan kwa mikwaju ya penalti, ambapo timu hiyo maarufu kama 'reds' hatimaye walifanikiwa kukamilisha urejeo wa ajabu.
Hiyo ilikuwa fainali ya Ulaya iliyofunga mabao mengi zaidi tangu mwaka wa1960, wakati Real Madrid ilipoizaba Frankfurt 7-3 mjini Glasgow.
Kwa Manchester City, ushindi utakamilisha mataji matatu ya kihistoria na hatimaye kuwapa taji moja ambalo wamekuwa wakilimezea mate kwa muda mrefu.
Inter Milan, kwa upande mwingine, wanawania taji la kwanza la Barani Ulaya tangu 2010, wakati Jose Mourinho alipowaongoza kutwaa ushindi wa ligi ya Mabingwa.
Safari ya City kuelekea Istanbul
City wamekuwa katika kila mashindano ya ligi ya mabingwa tangu msimu wa 2011-12, lakini bado hawajanyakua kombe hilo linalotamaniwa.
Pambano la Jumamosi ni fainali yao ya pili katika misimu mitatu, kufuatia kipigo cha 2021 kutoka kwa wapinzani wa Uingereza Chelsea huko Porto.
Kikosi cha Pep Guardiola kimekuwa na makali msimu huu na kitaingia uwanjani kama kipenzi kikuu.
City ilishinda Kundi G na kisha kuwapiku RB Leipzig katika hatua ya 16 bora, kwa ushindi wa mabao 7-0 kwenye mechi ya nyumbani ambayo mshambuliaji matata Erling Haaland alifunga mara tano.
Waliofuata ilikuwa Bayern Munich ya Ujerumani.
Mchezo wa mkondo wa kwanza nchini Ujerumani ulimalizika huku bao la Haaland likifutiliwa mbali na penalti iliyofungwa na Joshua Kimmich.
Katika mechi ya marudiano, City waligeukia mtindo huo na kuambulia ushindi mnono wa mabao 3-0 usiku huo dhidi ya Bayern Munich.
Changamoto yao kubwa, ilikuwa nusu fainali dhidi ya mabingwa watetezi Real Madrid. Mambo yalikuwa tofauti kabisa, hata hivyo, mabingwa hao wa Ligi ya Premia waliizaba Madrid 4-0 katika mechi ya kwanza wakiwa nyumbani,
Huku mechi ya ugenini ikiisha 1-1 na City ikajikatia tiketi yake jijini Istanbul kwa ushindi wa jumla ya 5-1.
Safari ya Inter kuelekea Istanbul
Inter Milan wana mvuto mkubwa wa Uingereza, wakijivunia mataji mfululizo mnamo 1964 na 1965, na walishinda taji lao la mwisho la ligi ya mabingwa mnamo 2010.
Fainali hiyo ilikuwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid, ambapo bao la kujifunga kutoka kwa mshambuliaji Diego Milito liliiwezesha Inter kushinda 2-0 dhidi ya Bayern Munich.
Msimu huu, timu ya Simone Inzaghi ilimaliza Kundi C katika nafasi ya pili, kabla ya kuzishinda Porto za Ureno na Benfica katika Raundi ya 16 na robo fainali, mtawalia.
Nusu fainali yao ilikuwa dhidi ya majirani, AC Milan, mechi ambayo walishinda kwa mabao matatu kwa bila katika michuano miwili.
Inter walimaliza wa tatu katika Ligi ya Serie A msimu huu, lakini walishinda Coppa Italia mwezi Mei, na watakuwa na hamu ya kuongeza taji kuu la Barani Ulaya katika mechi yao dhidi ya Manchester City.
Mabao mengi kwa City
Manchester City wanaongoza orodha ya wafungaji bora wa ligi ya mabingwa msimu huu wakiwa na mabao 31, mbele ya jumla ya mabao 19 ya Inter. Haaland ndiye mfungaji bora akiwa na mabao 12 na atakuwa tishio kubwa katika lango la goli la Inter Milan. Kwa Inter, mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko amefunga mabao manne Barani Ulaya msimu huu.