Mali, mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa dhahabu barani Afrika, imetoa hati ya kukamatwa kwa Mark Bristow, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold.
Hati ya kibali ilionekana siku ya Alhamisi na Reuters.
Hii inazidisha mzozo na kampuni ya uchimbaji madini ya Canada.
Serikali inayoongozwa na wanajeshi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi inatafuta mapato zaidi kutoka sekta hiyo ili kuimarisha mapato ya serikali.
Imewaweka kizuizini watendaji wakuu wa madini ili kuweka shinikizo kwa makampuni ya kigeni yanayofanya kazi huko.
Wafanyakazi wanne waandamizi wa ndani wa Barrick walizuiliwa kwa muda mfupi mwezi Septemba huku serikali ikidai takriban dola milioni 500 za kodi ambazo hazijalipwa, na kisha kukamatwa tena mwezi uliopita wakisubiri kesi.
Bristow aliiambia Reuters mapema mwezi wa Novemba kwamba kampuni yake ambayo ni mchimbaji dhahabu wa pili duniani ilikuwa na uhakika wa kusuluhisha madai na mizozo na mamlaka ya serikali kabla ya mwisho wa mwaka.
Kutakatisha pesa
Bristow anatuhumiwa kwa utakatishaji fedha na kukiuka kanuni za fedha, hati ya kibali, iliyoripotiwa kwanza na vyombo vya habari vya Mali tarehe 4 Disemba, ilionyesha.
Uhalisia wake ulithibitishwa na vyanzo viwili vilivyo karibu na suala hilo ambavyo viliomba visitajwe.
Barrick ilisema kampuni hiyo "haitatoa maoni" kuhusu hati ya kukamatwa iliyoripotiwa, ikijibu ombi la Reuters.
Hisa za Barrick zilikuwa chini kwa 2.9% kwenye soko la hisa la Toronto baada ya habari hii.
Bristow, raia wa Afrika Kusini ambaye huwa mara nyingi kati ya Uingereza na Marekani, alisafiri mara ya mwisho kwenda Mali mwezi Julai, kulingana na tovuti ya kampuni hiyo. Kampuni ya Barrick ina makao yake makuu mjini Toronto.