Jackie Maribe and Jowie Irungu accused of murder in Kenya

Mahakama nchini Kenya imempata na hatia ya mauaji Joseph Irungu maarufu Jowie aliyekuwa mpenzi wa mwanahabari Jackie Maribe. Jowie, amepatikana na hatia ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani mnamo Septemba 2018.

“Baada ya kuzingatia ushahidi wa shauri hili ni matokeo ya mahakama hii kuwa upande wa mashtaka umetoa ushahidi wa kutosha na umekidhi.... Ni matokeo ya mahakama hii kwamba mshtakiwa wa kwanza alimuua marehemu,” alisema jaji Grace Nzioka.

Kesi yake ilipata umaarufu zaidi nchini Kenya kwa sababu ya uhusiano wa kimapenzi kati ya Irungu na mwanahabari nchini Kenya Jacque Maribe ambaye pia alishtakiwa kwa mauaji hayo.

Mahakama imemuachia huru mwanahabari huyo.

"Ni maoni yangu kwamba shtaka lililoletwa dhidi ya mshtakiwa wa pili (Jacque Maribe) halikuwa shitaka sahihi," jaji Nzioka alisema.

Sababu za kumhukumu Irungu

Sababu ambazo jaji Nzioka alizitoa za kumpata Irungu na hatia ni pamoja na;

- Irungu alidanganya kuwa hakumjua Monica ilhali alimfahamu Monica Kimani kabla ya kifo chake. Jaji Nzioka anasema ushahidi unaonyesha walikuwa darasa moja katika Chuo Kikuu cha Kenya Polytechnic, alimtembelea nyumbani kwake na kuwasiliana kwenye mtandao wa Instagram.

-Kitambulisho alichotumia Irungu kuingia nyumbani kwa Monica kiliibiwa kutoka sehemu moja ambapo Jowie na Jacque waliishi siku mbili kabla ya mauaji hayo.

- Nguo zake zikiwa na damu zilizochafuliwa na kofia ya maroon zilitambuliwa na mashahidi watano tofauti.

- Jaji alisema anakubaliana na upande wa mashtaka kwamba bunduki ambayo Jowie alikuwa nayo wakati huo ilikusudiwa na kutumika kwa madhumuni ya kumtisha marehemu Monica.

- Nguo zake ikiwa ni kinyasa na kofia zilitambuliwa na mashahidi watano tofauti.

- Moja ya mashahidi ambao wanalindwa amesema kwamba Irungu alitoka nyumbani kwa Monica saa tano za jioni na hakuna mtu mwingine aliyekwenda kwenye nyumba hiyo.

- Jaji alisema kwamba hakuna mtu aliyemwona Jacque Maribe nyumbani kwa Monica.

TRT Afrika