Mkutano wa kimataifa wa kujadili swala la plastiki ambao utafanyika Nairobi wiki ijayo una nia ya kuunda sera ya kimataifa juu ya uchafuzi wa plastiki, pamoja na mazingira ya baharini.
Umoja wa matifa unaonya kuwa bila hatua za haraka, takriban tani milioni 11 za plastiki zinazoingia baharini kwa mwaka zitaongezeka mara tatu katika miaka ishirini ijayo.
Hii itamaanisha kati ya tani milioni 23 na 37 za plastiki zitatiririka baharini kila mwaka ifikapo mwaka wa 2040.
Wataalamu wanasema kuwa kuchakata tena hakuwezi kumaliza uchafuzi wa plastiki na kwamba ubinadamu unahitaji kutumika na kutoa nyenzo kidogo.
UN inasema kuwa zaidi ya tani bilioni 6.5 ya platiki inazunguka duniani na uchafuzi wa plastiki umepatikana katika kila mfumo wa ikolojia, ardhini na majini.
Inaongezea kuwa chembe ndogo ndogo za plastiki pia zimeripotiwa kupatikana katika sehemu ya miili ya binadamu, kwenye damu, na maziwa ya mama, na kusababisha vitisho kwa afya ya binadamu kutokana na viungio vya sumu katika bidhaa za plastiki.
Nchi 34 kati ya 54 barani Afrika zimepitisha sheria ya kupiga marufuku plastiki na kuitekeleza au kupitisha sheria kwa nia ya utekelezaji.
Kati ya hizo, 16 wamepiga marufuku kabisa mifuko ya plastiki au wamefanya hivyo kwa sehemu kadhaa lakini chnagmpoto ni kuwa bado nyingi hazijawasilisha sheria za kutekeleza marufuku hiyo.