Kwa Picha: Kenya kuanza kuzalisha pikipiki za umeme

Kwa Picha: Kenya kuanza kuzalisha pikipiki za umeme

Serikali inapanga kutoa angalau pikipiki 200,000 za umeme
Pikipiki za umeme nchi Kenya Picha / Rais William Ruto 

Rais William Ruto amevumbua mpango wa pikipiki za umeme.

"Lengo letu ni kuhimiza kupitishwa kwa nishati mbadala ambayo itaendana na hatua yetu ya mabadiliko ya hali ya hewa na kukuza ukuaji wa uchumi katika nchi yetu," Rais Ruto amesema.

Pikipiki za umeme nchi Kenya Picha/ Rais William Ruto 

Rais anasema pikipiki za umeme zitatoa usafiri wa bei nafuu na rafiki kwa mazingira.

Pikipiki za umeme nchi Kenya Picha/ Rais William Ruto 

Pikipiki hizi zinaunganishwa Roam Park, mojawapo ya viwanda vikubwa zaidi vya kuunganisha pikipiki za umeme katika Afrika Mashariki.

Pikipiki za umeme nchi Kenya Picha/ Rais William Ruto 

Rais Ruto anasema serikali inalenga kuzalisha pikipiki 200,000 za umeme katika sekta ya uchukuzi kufikia mwisho wa 2024.

Pikipiki za umeme nchi Kenya Picha/ Rais William Ruto 

Serikali pia imeamua kupunguza asilimia 16 ya ushuru kwa bei ya pikipiki za umeme.

TRT Afrika