Kanali Assimi Goïta aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka wa 2020 baada ya kumpindua aliyekuwa Rais wa wakati huo Ibrahim Boubacar Keïta.

Kiongozi wa kijeshi wa Mali amejipandisha cheo maalum cha jenerali wa jeshi: Kanali Assimi Goïta wa jeshi la nchi kavu - tuzo ya juu zaidi ya kijeshii ambayo inashikiliwa na wakuu wawili wa zamani wa nchi katika historia ya nchi hiyo.

Inakuja zaidi ya mwaka mmoja baada ya serikali ya kijeshi nchini Mali kupitisha katiba mpya ambayo inaongeza mamlaka ya rais na vikosi vya jeshi.

Tangazo hilo lilitolewa Jumatano na Baraza la Mawaziri, ambalo lilichapisha taarifa kwenye tovuti ya sekretarieti kuu ya serikali ya Mali.

Kanali wengine watano wenye ushawishi mkubwa wa jeshi la kijeshi la Mali pia walipandishwa cheo cha "kipekee" na kuwa majenerali wa nyota nne.

Mali ilishuhudia mapinduzi mawili katika miaka ya hivi karibuni, moja mnamo Agosti 2020 na nyingine Mei 2021.

TRT Afrika