RAis wa Kenya Willima Ruto ameongoza wananchi kuadhimisha siku ya taifa ya kupanda miti / Picha: Ikulu Kenya

Wakenya wa tabaka mbalimbali wanahimizwa na seriklia kujitokeza kupanda miti huku Mei 10 ikitangazwa kama siku ya taifa ya kupanda miti.

Mwaka huu siku hii inafanyika huku nchi ikiendelea kuathiriwa na mafuriko katika sehemu tofauti za nchi.

Gazeti ya serikali imetangaza uamuzi huo "kwa kutambua kwamba athari za mabadiliko ya hali ya hewa ni tishio la nje kwa usalama wa taifa na usalama wa umma na uendelevu wa ikolojia ya Kenya."

Serikali imetenga siku hii pia kuwakumbuka waliathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi. Kwa sasa mafuriko kutoka Aprili 2024 yameua zaidi ya watu 200, huku yakiharibu mali za watu na kuwalazimisha wengi kuhama makwao.

"Hii itasaidia kukuza juhudi za upandaji miti katika maeneo yenye mafuriko ili kuunga mkono juhudi zinazoongozwa na jamii za kupanda miti kwa kutumia kampeni ya miti bilioni 15.

Huu ni mwaka wa pii wa Kenya kufanya hafla hii ya kitaifa, ambapo ya Kwanza ilifanyika mwezi Novemba 2023.

"Leo, Mbuga ya Kitaifa ya Aberdare, kwa ushirikiano na Old Mutual itapanda zaidi ya miti 10,000 ya kiasili! Kila mti huhesabiwa katika safari yetu kuelekea mfumo wa ikolojia unaostawi," Huduma ya wanyama pori ya kenya , KWS imesema katika akaunti yake ya X.

Rais William Ruto alianzisha mradi wa kupanda miti akilenga miti bilioni 15 kufikia mwaka wa 2032 Disemba 2022.

Hatua hii alisema inalenga kupunguza utoaji wa hewa mkaa, kukomesha na kurudisha nyuma ukataji miti na kurejesha hekta milioni 5.1 za ardhi iliyomomonyoka na kuharibiwa katika sehemu tofauti za nchi.

Machi 2023 mke wa Rais wa Kenya, Rachel Ruto alitwaa hekta 200 katika Msitu wa Ikweta wa Kakamega, katika jitihada zake za kuimarisha upandajii wa miti nchini Kenya.

TRT Afrika