Serikali ya Rais William Ruto imelazimika kupunguza bajeti katika sekta tofauti baada ya maandamano nchini/ Picha: Ikulu Kenya 

Rais William Ruto wa Kenya aliidhinisha muswada wa mapato ya ziada Jumatatu baada ya kupitishwa na Bunge la Kitaifa Julai 31, 2024.

Hii inafuatia Muswada ya Fedha 2024 ambao haikusainiwa na rais Ruto baada ya maandamano ya Juni 2024.

Licha ya vikwazo vya kifedha, sheria mpya hulinda matumizi muhimu, ikiwa ni pamoja na takriban kiasi cha KSh20 bilioni ( zaidi ya $154 milioni) kusaidia wakulima na kuimarisha uzalishaji na tija.

Ili kusaidia mageuzi ya elimu, Sheria ya Uidhinishaji wa Ziada imetenga KSh120.7 bilioni, ikijumuisha uthibitisho wa walimu wote wa Shule ya Sekondari ya Vijana, na KSh31.3 bilioni kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

Zaidi ya hayo, Muswada ambao Rais alitia saini kuwa sheria umetenga KSh16.2 bilioni kufadhili mageuzi ya sekta ya afya na kukuza Huduma ya Afya kwa Wote.

Makato makubwa kwa bajeti

Serikali ya Rais Ruto imekata bajeti katika sekta tofauti ya thamani ya Kshs. 145 billioni ambayo ni zaidi ya $1.12 bilioni.

- Ofisi ya Rais Kshs. 139.81 billion ($1.08 bilioni)

- Bunge: Kshs. 3.7 billion ($28.4 milioni)

- Mahakama: Kshs. 2.1 billion ($16.2 milioni)

- Ikulu/ naibu wa rais: Kshs. 6 billion ($46.1 milioni)

- Hazina ya Taifa: Kshs. 7 billioni ($53.8 milioni)

- Miradi ya Afya: Kshs. 6.9 billioni ($53milioni)

- Barabara na Usafiri Kshs. 17.3 billioni ($133 milioni)

Nyongeza ya mishahara ya maafisa wa usalama pia imezingatiwa, huku sheria mpya ikitenga KSh3.5 bilioni ( $26.9 milioni) kwa ajili ya kuimarisha malipo ya maafisa wa polisi wanaohudumu katika mashirika mbalimbali.

TRT Afrika