Mabadiliko katika sheria ya mabadiliko ya tabianchi ina nia ya kudhibiti masoko ya kaboni/ Picha kutoka Ikulu ya Kenya 

Rais William Ruto ameidhinisha Mswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Tabia nchi ambao ulichapishwa Julai.

Sheria hiyo ina nia ya kudhibiti masoko ya kaboni.

"Mswada huu unarekebisha Sheria ya Mabadiliko ya Tabia nchi, 2016, inayotoa udhibiti wa masoko ya kaboni kando na kuimarisha jinsi ya kukumbana na mabadiliko ya hali ya hewa," Ikulu ya Kenya imesema.

Sheria ya awali ya 2016 haikuwa na mfumo wa kisheria wa biashara ya kaboni.

Mabadiliko katika sheria hii unatoa miamala katika biashara ya kaboni kama inavyotekelezwa chini ya sheria kwa ajili ya kupunguza uzalishaji wa gesi inayochafua mazingira.

Kulingana na sheria hii , sasa waziri anaruhusiwa kufanya makubaliano ya nchi mbili au ya kimataifa ya biashara ya kaboni, akipata idhini kutoka kwa mawaziri.

Sheria mpya zaidi inaagiza mikataba ya maendeleo ya jamii ambayo lazima ijumuishe mchango wa kijamii wa kila mwaka kutoka kwa mradi wa biashara ya kaboni.

Inapendekeza jamii husika kupata asilimia 40 kila mwaka kwa miradi ya ardhi na asilimia 25 kila mwaka kwa miradi isiyo ya ardhi.

TRT Afrika