Kenya imeanza kutimiza marufuku ya karatasi za takataka ambayo ni hatari kwa mazingira .
Mamlaka ya kitaifa ya usimamizi wa mazingira, NEMA imesema katika taarifa ya Julai 8, 2024
"Kuhakikisha usimamizi mzuri wa mazingira wa maji ya kikaboni, mamlaka inaagiza kwamba ndani ya siku 30 kutoka kwa taarifa hii taka zote zinazozalishwa na kaya na taasisi za sekta ya umma zitatengwa na kuwekwa kwenye mifuko ya takataka inayoweza kuvundishwa na bakteria au biodegradable kwa asilimia 100," NEMA imesema katika taarifa.
Wananchi wamearifiwa kutochanganya uchafu huo wa oganiki na uchafu aina nyingine kwani utapelekwa sehemu maalumu kwa ajili ya usindikaji zaidi.
"Matumizi ya karatasi ya plastiki ya kawaida kwa ajili ya kuwekea uchafu umesitishwa mara moja," NEMa ineongezea.
Watoa huduma wenye jukumu la kuokota taka wametakiwa kutoa karatasi zinazofaa za taka kwa wananchi ili kuwawezesha kutimiza masharti hayo mapya yenye kulenga usafi wa mazingira.
Mwaka wa 2017 serikali ya Kenya ilipiga marufuku uzalishaji, ununuzi kutoka nchi za nje na matumizi ya karatasi za plastiki na zile zinazotumiwa kuwekea bidhaa.