Maziwa yanayodaiwa kuwa ya magendo kutoka Uganda, Uchina na New Zealand/ Picha kutoka DCI Kenya.

Maafisa wa upelelezi nchini Kenya wamewakamata wauzaji wa unga wa maziwa magendo na zaidi ya tani 32.5 za bidhaa hiyo kwenye maeneo ya hifadhi ya Eastleigh jijini Nairobi nchini Kenya.

"Katika oparesheni hiyo kali, wakala mmoja asiyejulikana huko Eastleigh kwa jina la Ali Noor aliwaelekeza polisi kwenye eneo la hifadhi ya siri katika eneo la Kamakis kando ya Eastern Bypass, baada ya yeye (afisa) kujifanya kama mnunuzi," kitengo cha DCI Kenya kimeelezea.

Kenya ina sheria zinazodhibiti bidhaa za magendo ambazo zinalaumiwa kuumiza uchumi kutokana na kuwepa ushuru,

Kitengo hicho kinasema gari ya mizigo yenye shehena ya mifuko 150 ililetwa ambapo kila mfumo ulikuwa na uzito wa kilo 25.

Bei iliyokubaliwa ilikuwa ni dola 105 kwa kila mfuko, na hapo mnunuzi aliambiwa alipe dola 15,739 katika shughuli hiyo.

Bunge la Kenya lilipitisha sheria ya kupambana na bidhaa bandia mwaka 2008 ili kupiga marufuku biashara ya bidhaa ghushi na kuanzisha Mamlaka ya Kupambana na Bidhaa Bandia.

Mashirika ya kitaifa, kikanda na kimataifa yanayohusika katika kupambana na bidhaa bandia huja pamoja kwa mujibu wa sheria ili kuunganisha nguvu na kukuza ushirikiano baina ya mashirika ili kupiga vita biashara hii inayoonekana kustawi.

Maafisa wa upelelezi nchini Kenya wamewakamata wauzaji wa unga wa maziwa magendo/ Picha kutoka DCI Kenya

Wapelelezi wengine waliwavamia washukiwa hao wawili lakini dereva wa gari alitoroka.

Wapelelezi wanasema walipata mifuko mengine 1150 ambapo kila mmoja ulikuwa na uzito wa kilo 25 za unga wa maziwa na mifuko 289, kila mmoja ukiwa na uzito wa kilo 25 za wanga wa mahindi.

Chapa za unga ya maziwa hayo ya magendo ni pamoja na Fresh Dairy ya Brookside Uganda, Gardo Non Dairy Creamer ya Uchina, SAMA ya New Zealand, Lato ya Uganda & magunia 289 ya bidhaa ya wanga ya mahindi ya India.

DCI anasema washukiwa wamewekwa chini ya ulinzi huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

TRT Afrika