Kenya imependekeza miswada mitatu ya kuboresha afya/ Picha : Other 

Serikali imeanzisha mchakato wa kufuta Mfumo wa Taifa wa Bima ya Hospitali (NHIF) katika hatua inayolenga kutoa huduma ya afya kwa wote nchini.

Uamuzi huu umefanywa na mkutano wa baraza la mawaziri uliokutana na rais William Ruto Jumanne.

Badala yake serikali imependekeza miswada mipya ya sheria ya afya: Hazina ya Afya ya Msingi; Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii; na Mfuko wa Dharura, Ugonjwa wa Muda Mrefu na Muhimu.

Ujumbe uliotolewa na Msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed ulionyesha kuwa Miswada hiyo; Mswada wa Sheria ya Huduma ya Afya ya Msingi, 2023; Mswada wa Sheria ya Afya ya Kidijitali, 2023; Mswada wa Sheria ya Ufadhili wa Uboreshaji wa Kituo, 2023; na Mswada wa Bima ya Afya ya Jamii, 2023 utafikishwa bungeni ili kuidhinishwa.

"Miswada hii inaleta dhana katika mfumo wa kisheria na kitaasisi wa huduma ya afya nchini Kenya kwa kufuta hazina ya sasa ya bima ya afya ya kitaifa na kuanzisha mifumo hizi tatu," Baraza la Mawaziri lilisema katika taarifa.

Msemaji wa rais, Hussein Mohammed, amesema kuwa mifumo hiyo tatu inatokana na upangaji upya wa fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya bima ya afya.

"Mifumo hii mipya tatu zinatokana na upangaji upya wa fedha zilizokuwepo awali, yaani, upangaji upya wa zaidi ya dola bilioni tatu ambazo zinajumuisha matumizi yetu ya afya, ili kufikia bima ya afya kwa wote. Mfumo wa Huduma ya Msingi utafadhiliwa kutoka Hazina," Hussein alisema katika mtandao wake wa X.

Hata hivyo alibainisha kuwa mfumo wa huduma ya msingi utafadhiliwa na hazina ya taifa.

Mswada wa kidijitali wa afya unalenga kuboresha huduma ya afya ya kidijitali.

TRT Afrika