Na Coletta Wanjohi
TRT Afrika, Istanbul, Uturuki
Kwa Wakenya na wageni wengine kutoka nje ya nchi, Wikiendi imejipanga, sherehe imejileta nchini Kenya huku dunia ikiangazia nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika mashindano maarufu ya magari, World Rally Championship.
Mashindano ya magari ya dunia, ambayo pia yanaitwa Kenya Safari Rally yanafanyika kuanzia 28 hadi 31 Machi 2024, mjini Naivasha.
Baada ya mapumziko ya wiki sita tangu mashindano ya Uswidi, madereva na timu sasa wanakabiliwa na changamoto tofauti kabisa kwani awamu ya tatu ya msimu ikianza Alhamisi katikati ya tambarare zinazovutia na wanyamapori wa Kiafrika, nchini Kenya.
Rais William Ruto amezindua rasmi mashindano hayo jijini Nairobi.
"Tutaunganisha juhudi na ubingwa wa dunia wa rally ili kuweka Safari Rally kama mchezo wa kiwango cha kimataifa. Hii itakuza utalii wetu na ukuaji wa uchumi kwa ujumla," rais Ruto alisema.
Safari Rally ya mwaka huu imesogezwa nyuma kimkakati katika kalenda ili kurejesha nafasi yake ya kihistoria ya Machi, ikiwiana kikamilifu na msimu wa mvua wa Kenya.
Mvua za kabla ya mashindano zimesababisha kuwepo kwa matope katika baadhi ya barabara wakati wa mapumziko, na magari mengi yanatumia chombo cha kusaidia injini kuendelea "kupumua" ili kukabiliana na sehemu zinazoweza kujaa maji.
Macho yote yako kwenye timu ya Toyota Gazoo. Timu ya GR Yaris Rally1 ambayo imeshinda kila toleo tangu 2021, na hata kudai ushindi mkubwa wa nne bora miezi 12 iliyopita.
Licha ya rekodi yake ya kutisha, hata hivyo, Toyota bado inatafuta ushindi wake wa kwanza wa msimu huu.
Elfin Evans, Takamoto Katsuta na bingwa wa dunia anayetawala Kalle Rovanperä kila mmoja watakuwa na matumaini ya kubadilisha hilo.
Rovanperä aliongoza jukwaa mwaka wa 2022, wakati Katsuta - ambaye anatoka Japan - amepata majukwaa mawili ya kuvutia kutoka kwa mashindano matatu ya mwanzo.
Hyundai Motorsport nayo iko tayari kupinga ukuu wa Toyota Afrika, na kupanua mfululizo wake wa mafanikio kwa kutumia madereva wa i20 N Thierry Neuville, Ott Tänak na Esapekka Lappi.
Mshindi wa Rallye Monte-Carlo Neuville kwa sasa anaongoza ubingwa wa madereva kwa pointi tatu kutoka kwa Evans, huku Lappi mwenye hamu ya ushindi aliandikisha ushindi wake wa pili wa maisha mara ya mwisho akiwa Uswidi.
M-Sport Ford inaingia Kenya kwa kasi baada ya Mfaransa Adrien Fourmaux kufunga jukwaa lake la kwanza katika raundi ya awali.
Timu ya Uingereza inawapa magari matatu ya Puma Rally1 kwa Fourmaux, Grégoire Munster na dereva bwana Jourdan Serderidis.
Mashindano hayo yameanza katika jiji kuu la Nairobi siku ya Alhamisi.
Yatapita katika hatua 19 za kuchosha kuzunguka Ziwa Naivasha na Elmenteita zinazochukua kilomita 367.76 kabla ya Jumapili kukamilika huko Naivasha.
Utalii ndani ya mashindano
Mashindano haya huwa fursa kubwa ya Kenya kuuza utalii wake.
Madereva na timu wanakabiliwa na changamoto katikati ya tambarare zinazovutia na wanyamapori wa Kenya.
Jinsi madereva wanavyojaribu kukabiliana na hali inaongeza msisimko kwa mashabiki. Mashindano mwaka huu yataanzia Mjini Nairobi na kuelekea eneo la Naivasha.
Ziwa Naivasha, na mto Elementatita zitawaangazia madereva na mashabiki watakaokuwa wamejitokeza.
Mashindano yatapita Ziwa Naivasha ambalo ni kubwa kuliko yote ya Bonde la Ufa Kenya, na Mbuga ya wanyama la Hell's Gate.
Mashindano yatapita katika Hifadhi ya Wanyamapori ya Oserian ambayo ni makazi ya chui, Beisa Oryx, duma, faru mweupe na zaidi.
Kuna ripoti kuwa hoteli za kitallii tayari zimejaa huku wahudumu tofauti wakijipatia biashara.
Rally si rally bila sherehe, hivyo ndivyo Wakenya wanavyosema.
Kwa hivyo, matamasha tofauti ambayo yatakuwepo mjini Naivasha usiku na mchana kuanzia tarehe 27 to 31 Machi, yatawavutia wengi kutaka kutembelea Naivasha au Kenya tena hata baada ya Rally.