Rais William Ruto wa Kenya, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga wakiwa katika shamba ya Museveni nchini Uganda/  Picha : Rais William Ruto 

Rais wa Kenya Wiliam Ruto ameanza kampeni ya Kenya kupata kiti cha uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

Kiongozi wa Muungano wa Kisiasa wa Azimio Raila Odinga ndiye ambaye ameteuliwa na Kenya kugombea nafasi hiyo.

Rais William Ruto akiwa na Raila Odinga walimtembelea rais wa Uganda Yoweri Museveni Jumatatu kwa ajili ya kuomba uungwaji mkono na Uganda.

"Pia kilichojadiliwa ni tangazo la kugombea kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya nafasi ya uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika," Rais William Ruto alisema katika mtandawo wa X.

Rais William Ruto wa Kenya, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga wakiwa katika shambani kwa Museveni nchini Uganda/ Picha: Rais William Ruto 

Waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga naye akathibitisha maongezi hayo.

"Tulijadili pia kugombea kwangu Uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika," Odinga alisema katika mtandao wa X. "Ninamshukuru sana Rais Museveni kwa kuidhinisha kwa dhati kuteuliwa kwangu na kwa Rais Ruto kwa kuunga mkono kikamilifu uteuzi wangu," aliongezea.

Kenya inatakiwa kuanza kufanya kampeni kwanza kwa majirani zake ili ipate uungwaji mkono mzuri ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nafasi ya mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika ni nafasi ya mtendaji mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika, ambae pia ni mwakilishi wa kisheria wa AU na Afisa Mkuu wa Uhasibu wa Tume.

Nafasi hiyo kwa sasa, ipo chini ya Moussa Faki Mahamat ambae ni raia wa Chad, ambae aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo. Awamu yake ya pili ya uongozi inakwisha mwaka huu 2024.

Ili kupata kiti hiki, marais wa nchi za Afrika hupiga kuwa ya siri. Mgombea anahitaji kupata angalau theluthi mbili ya kura, ambayo ni sawa na kura 36, ​​ili kutangazwa mshindi.

Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo ameunga mkono uamuzi huo wa Raila Odinga.

Hii sio mara ya kwanza kwa Kenya kugombea nafasi hiyo ambayo ni kubwa katika bara la Afrika. Mwaka 2017, Kenya ilijaribu kupata nasafi hiyo ya juu kupitia mwanasiasa wake Amina Mohammed, aliyekuwa wakati huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya.

Hata hivyo, Kenya ilishindwa na Chad iliyowakilishwa na Mwenyekit wa sasa Moussa Faki Mahamat.

Raila amewahi kutoa huduma ya kibara.

Aliteuliwa kuwa Mwakilishi Mkuu wa Maendeleo ya Miundombinu katika Tume ya Umoja wa Afrika mwaka wa 2018. Majukumu hayo yalikwisha Februari 2023.

TRT Afrika