Wafanyikazi hao waliajiriwa na wanakandarasi wa ndani kukagua machapisho kwenye Facebook. /Picha: Reuters

Mahakama ya Kenya iliamua siku ya Ijumaa kwamba kampuni mama ya Facebook Meta inaweza kushtakiwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki kutokana na kufukuzwa kazi kwa wakaguzi wa maudhui na mwanakandarasi.

Mwaka jana wakaguzi wa maudhui walishtaki Meta na wanakandarasi wawili wa ndani, wakisema walipoteza kazi zao na Sama, kampuni ya Kenya yenye kandarasi ya kugagua maudhui ya Facebook, kwa kuandaa muungano.

Walisema waliwekwa kwenye orodha ya waliopigwa marufuku baada ya kutuma maombi ya kutafuta kazi yenye majukumu sawa katika kampuni nyingine, Majorel, baada ya Facebook kubadilisha wakandarasi.

Mazungumzo ya kupata suluhu nje ya mahakama hayakuzaa matunda mwezi Oktoba mwaka jana.

Maamuzi yamethibitishwa

Uamuzi wa Ijumaa wa Mahakama ya Rufaa uliidhinisha uamuzi wa awali wa mahakama ya wafanyikazi ya Kenya mnamo Aprili 2023 kwamba Meta inaweza kukabiliwa na kesi kuhusu kufutwa kazi kwa wakaguzi wa maudhui, ambayo Meta ilikata rufaa.

Pia ilikubali uamuzi tofauti mnamo Februari 2023 kwamba Meta inaweza kushtakiwa nchini Kenya kwa madai ya mazingira duni ya kazi, ambayo Meta pia ilikata rufaa.

"Hitimisho 'a matokeo yetu hapo juu ni kwamba rufaa za Meta, hazina mashiko na rufaa zote mbili zimetupiliwa mbali na gharama kulipwa kwa walalamikiwa," majaji watatu wa Mahakama ya Rufani walisema katika uamuzi wao siku ya Ijumaa.

Reuters