Jumla ya majina 20 yalipendekezwa na Rais William Ruto, kisha kupelekwa Bungeni kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano.
Mchakato huo wa siku nne ulishuhudia jina la Stella Soi Lang'at likirudi, baada ya kamati ya uteuzi ya Bunge la nchi hiyo kutoridhishwa na majibu yake wakati wa mahojiano ambaye hakuridhisha kamati ya bunge ya uteuzi katika mahojiano yake.
Langa't alikuwa amependekezwa kuongoza Wizara ya Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Urithi lakini hakuweza kuidhinishwa baada ya kushindwa kuishawishi kamati ya bunge kubeba jukumu hilo.
Katika ripoti yake, kamati ya Bunge ilidai kuwa Stella Soi Lang'at hakuwa na uelewa wa majukumu yake tarajiwa.
"Mteule hafai kwa nafasi aliyoteuliwa kwani hakuweza kujibu kwa njia ya kuridhisha maswali yaliyoulizwa wakati wa kusikilizwa kwa uidhinishaji unaohusiana na Jinsia, Urithi na Utamaduni," Wabunge walisema kwenye ripoti hiyo.
Kwa mujibu wa wabunge hao, Wizara hiyo ni ya kimkakati kwani inasimamia sera, huduma muhimu za kitaifa.
Walisema kuwa Wizara inahitaji uongozi wenye dira madhubuti ya kimkakati, usikivu wa kitamaduni, na uelewa wa kina wa usimamizi wa sera, jambo ambalo Langat alikosa.
Kulingana na kamati hiyo, mtu wa kuongoza kamati hiyo anapaswa kuwa mzungumzaji mahiri na mbunifu na mwenye nia ya kukuza turathi za kitamaduni na usawa wa kijinsia.
"Mteule alishindwa kuonesha sifa zozote kati ya hizi kwa kuridhika na kamati," wabunge walisema katika hotuba yao ya kumalizia na kuhitimisha hatima yake.
Wabunge hao pia walisema kuwa uzoefu wa miaka 30 wa Langat katika utumishi wa umma,unaangaziwa na mabadiliko ya mara kwa mara ya kazi katika majukumu mbalimbali.
" Majukumu yote ya kazi katika maeneo sita alipokuwa hayakuhitaji yeye kufanya mipango ya muda mrefu. kwa hivyo hajakuwa na uzoefu wa muda mrefu sana katika nafasi yoyote wakati wake wa kazi,"
Kamati ilisema Rais William Ruto anatarajiwa kuteua mtu mwingine atakayezingatiwa kwa wadhifa huo.