Paul Nthenge Mackenzie alikamatwa Aprili mwaka jana baada ya miili kugundulika ndani ya msitu wa Shakahola karibu na Bahari ya Hindi, / Picha: AFP

Mahakama nchini Kenya siku ya Alhamisi imemtia hatiani Paul Mackenzie na wenzake 94 kwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 400.

Hata hivyo, Mchengaji Mackenzie na wenzake walikana mashitaka hayo, yakiwemo kuchochea 'itikadi kali' kati ya wafuasi wake pamona na 'uhalifu wa kupangwa', kulingana na stakabadhi za mahakama ya Mombasa.

Mackenzie anadaiwa kuwachochea wafuasi wake kushinda njaa ili wamwone 'Yesu', tukio lililoushangaza ulimwengu.

Kiongozi huyo wa Good News International Church alikamatwa Aprili mwaka jana, baada ya miili kugunduliwa katika msitu wa Shakahola uliopo Pwani ya Kenya, huku uchunguzi wa maiti ukionyesha kuwa wengi wa waathirika hao wapatao 429 walipoteza maisha yao kwa njaa, kufuatia maelekezo ya Mackenzie.

Waathirika wengine, wengi wakiwa watoto walionekana na makovu shingoni na sehemu zingine za mwili, ikiashiria kuwa walinyongwa au kupigwa vibaya na kusababisha vifo vyao.

Ilimchukua muda kwa Mackenzie kujua siku na hatma yake Mahakamani Mombasa, baada ya upande wa mashtaka kuomba muda zaidi wa kuchunguza kesi hiyo.

Hata hivyo, ilitishia kumwachia huru dereva wa zamani wa teksi, iwapo mashitaka dhidi yake hayatowasilishwa ndani ya siku 14.

Kesi hiyo ya kushtua, iliyobatizwa 'mauaji ya msitu wa Shakahola', ilipelekea Serikali ya Kenya kutaka udhibiti mkubwa wa madhehebu ya dini mbalimbali nchini humo.

TRT Afrika