Mahakama ya juu nchini Kenya siku ya Jumanne ilibatilisha uamuzi wa kihistoria wa mahakama ya chini, na kutangaza kuwa Sheria ya Fedha ya 2023 yenye utata kuwa ya kikatiba.
Hapo awali Mahakama ya Rufaa ilitangaza kitendo hicho kuwa kinyume na katiba, ikitaja dosari katika mchakato wa ushirikishwaji wa umma uliopelekea kupitishwa kwake.
Hata hivyo, Mahakama ya juu, katika uamuzi wake, haikukubaliana na uamuzi huo, ikisema kuwa umma ulishauriwa vya kutosha na maoni yao kuzingatiwa wakati wa mchakato wa kutunga sheria.
"Tunaona kwamba maslahi ya umma yanaegemea kutoa amri za kulinda uthabiti katika mchakato wa bajeti na ugawaji ikisubiri kuamuliwa kwa kesi ya rufaa serikali," Mahakama ya Juu iliamua.
Uamuzi huo umezua hisia tofauti, huku serikali ikiukaribisha kama ushindi kwa sera zake za kifedha, huku Wakenya wengine wakisalia na wasiwasi.
Viongozi wa upinzani na mashirika ya kiraia wameelezea kusikitishwa na wasiwasi wao.
Wakosoaji wanadai kuwa sheria hiyo inaweka mzigo usiostahili kwa Wakenya wa kawaida, haswa kwa kuzingatia gharama ambayo tayari iko juu ya maisha na hali ngumu ya kiuchumi.
Uamuzi huo pia unatarajiwa kuibua mjadala wa umma na uwezekano wa kusababisha maandamano mapya. Kulingana na Mahakama ya Juu, rufaa hio itasikilizwa mwezi ujao wa Septemba.