Huku suala kubwa la matumizi mabaya ya dawa za kulevya na pombe, likiendelea kuwa sugu nchini Kenya. Wizara ya Afya imetangaza dhamira yake isiyoyumba katika kushughulikia tatizo hili hatari.
Akisisitiza athari kubwa kwa jamii, Waziri wa Afya Nakhumicha Wafula aliangaza hitaji la dharura la kuingilia kati.
"Matumizi mabaya ya dawa za kulevya na vileo sio tu huathiri mfumo wetu wa afya, bali pia husababisha madhara makubwa katika jamii," alisema Waziri Nakhumicha wakati wa kongamano la matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya katika mkoa wa Pwani. Kongamano hilo lililoongozwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua, Jumatatu.
"Kutoka mimba za utotoni hadi ukiukaji wa kingono na kijinsia na kuenea kwa virusi vya Ukimwi, madhara yake ni makubwa."
Serikali ilitenga zadi ya dola milioni 526 mwaka jana kwa ajili ya kupinga usambazaji wa magonjwa haya.
Waziri wa Afya ametangaza kuungana na wizara nyengine na mashirika ya usalama kuhakikisha kuwa maduka ya dawa yasiyofuata kanuni yanafungwa.
Tayari operesheni hii inaendelea ikiongozwa na Bodi ya Madawa na Sumu. Hii ni Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa.
Februari 18, mwaka huu, bodi hii ilitangaza kukamatwa kwa takriban watu 129 na maduka yao kufungwa katika msako dhidi ya maduka haramu ya madawa.
Zaidi ya katoni 200 za dawa haramu zilikamatwa. Msako ulifanyika katika maeneo ya mjini mkuu wa Nairobi na mikoa ya kusini na kaskazini ya nchi .