Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille akiwasili kwa mkutano na waandishi wa habari pamoja na Rais wa Kenya William Ruto wakati wa ziara yake katika Ikulu ya Nairobi, Kenya, Oktoba 11, 2024. / Picha: Reuters

Viongozi wa Kenya na Haiti wamewataka washirika wa kimataifa kuheshimu ahadi yao kwa misheni ya kulinda amani unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Haiti, wakisema kuwa misheni hiyo inahitaji rasilimali zaidi na kwamba bajeti yake itaisha Machi 2025.

Kenya, ambayo inaongoza kwa kutuma misheni ya kukomesha ghasia za magenge katika taifa hilo la Caribbean, imetuma karibu maafisa 400.

Wanaungana na takriban na maafisa wa polisi na wanajeshi kutoka Jamaica, lakini idadi hiyo inapungua kwa kiasi kikubwa kuliko 2,500 walioahidiwa na nchi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Chad, Benin, Bangladesh na Barbados, kwa misheni hiyo.

Rais wa Kenya William Ruto, ambaye alikutana na Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille mjini Nairobi siku ya Ijumaa, alisema Kenya itapeleka maafisa 600 zaidi mwezi ujao.

Umoja wa Mataifa umetoa ahadi za dola milioni 85 kwa misheni hiyo, ambapo dola milioni 68 hadi sasa zimepokelewa.

"Tuna fursa ya kufanikiwa ambayo inadhihirika kutokana na oparesheni ambazo tayari zimetekelezwa," Ruto alisema.

Conille aliwaomba washirika wa kimataifa kutuma maafisa ambao wameahidi kuhakikisha "kikosi kutoka Kenya kina rasilimali zinazohitajika".

Conille alisema mikutano yake ya kawaida na kamanda wa Kenya ilijaa maneno ya kutia moyo kwamba vita dhidi ya magenge ya Haiti "ni vya kushinda".

Magenge nchini Haiti yamezidi kuwa na nguvu tangu mauaji ya Julai 7, 2021 ya rais Jovenel Moise na sasa yanakadiriwa kudhibiti hadi asilimia 80 ya mji mkuu.

Kuongezeka kwa mauaji, ubakaji na utekaji nyara kumesababisha ghasia za makundi ya raia.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura kwa kauli moja mapema mwezi Oktoba kuongeza muda wa kikosi cha kimataifa kinachoongozwa na Kenya, baada ya kupuuzilia mbali wito wa Haiti wa kuanza mazungumzo ya kuigeuza kuwa misheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.

TRT World