Gari la kijeshi linapita karibu na watu wanaosherehekea huko Port Gentil nchini Gabon / Picha: Reuters

Mamia ya watu waliingia katika mitaa ya mji mkuu wa Gabon Libreville siku ya Jumatano kusherehekea baada ya maafisa wa kijeshi katika nchi hiyo inayozalisha mafuta kusema kuwa wametwaa mamlaka na kumweka rais Ali Bongo katika kifungo cha nyumbani.

Wananchi wa Gabon washerehekea katika mitaa Gabon/ Picha : Reuters 

Katika tangazo kwenye televisheni, usiku wa kuamkia Jumatano, maafisa kadhaa wa majeshi, walitangaza kuwa matokeo ya uchaguzi yamefutwa, mipaka ilifungwa na taasisi za serikali zilivunjwa.

Walisema wanawakilisha vikosi vyote vya ulinzi na usalama vya Gabon.

Wananchi wa Gabon wakiwa mitaani / Picha: Reuters 

Haya ni mapinduzi ya nane ya kijeshi katika Afrika Magharibi na Kati tangu 2020.

Gabon ni nchi inayopatikana katika eneo la Afrika ya Kati na inashiriki mpaka na Kongo Brazzaville, Equatorial Guinea na Cameroon.

Wananchi wa Gabon mitaani / Picha : Reuters 
TRT Afrika