Karne ya Uturuki itakuwa ni karne ya wanawake, Rais Recep Tayyip Erdogan amesema.
Akihutubia hafla iliyofanyika Istanbul kuadhimisha Siku ya Kupambana na Udhalilishaji Dhidi ya Wanawake Jumamosi, Erdogan amesema wanatekeleza sera ya kutokomeza vurugu dhidi ya wanawake kama sera ya taifa.
“Tunaamini kwamba, Bodi ya Kuratibu Vurugu Zinazofanywa dhidi ya wanawake, ambayo tumeianzisha na mtaala wetu mpya, wanaendesha shughuli ambazo zinathamani kwa Karne yetu ya Uturuki,” amesema katika Chuo Kikuu cha Halic.
Lengo, amesema, ni kujenga uelewa wa unyanyasaji dhidi ya wanawake, na kuongeza kwamba, Uturuki imefikia hatua kubwa katika hilo.
"Tutajenga pamoja Uturuki iliyo huru kutokana na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake kwa mshikamano na wanaume, wanawake, na vijana na wazee,” ameongeza.
Erdogan pia amesema kwamba wanatoa ulinzi wa taifa kwa wanawake wanaokabiliwa na unyanyasaji kwa kuwapa makazi, na kuwafuatilia na kwamba vituo vinavyotoa huduma hizo za kijamii vinapatikana Uturuki kote.