Pia kamati hiyo ilitoa wito wa kusimamishwa kwa "uwepo wa makampuni nchini Kenya hadi kuwe na mfumo wa kisheria wa udhibiti wa data za siri/ Picha Reuters

Jopo la bunge la Kenya lilitoa wito kwa mdhibiti wa teknolojia ya habari nchini humo Jumatatu kuzima utendakazi wa mradi wa cryptocurrency Worldcoin ndani ya nchi hadi kanuni kali zaidi zitakapowekwa.

''Mamlaka ya Udhibiti ya Mawasiliano ya Kenya inapaswa kuzima mifumo ya mitandaoni ya kampuni za Tools for Humanity Corp na Tools for Humanity GmbH Ujerumani (Worldcoin) ikiwa ni pamoja na kuorodhesha kama ilani anwani za IP za tovuti zinazohusiana," jopo la wabunge 18 lilisema katika ripoti.

Worldcoin ilizinduliwa katika nchi mbalimbali duniani na Tools for Humanity, kampuni iliyoanzishwa kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Open AI Sam Altman. Pia imekuwa chini ya uchunguzi nchini Uingereza, Ujerumani na Ufaransa.

Mradi huo bado unaweza kupatikana kupitia Mtandao, hata baada ya kusimamishwa mwezi Agosti.

Wakati wa kusimamishwa kwa ukusanyaji wa data mwezi Agosti, mamlaka ilisema mbinu ya mradi ya kupata kibali cha watumiaji kama malipo ya tuzo ya fedha ya zaidi ya $50 wakati huo ilipakana na ushawishi.

Pia kamati hiyo ilitoa wito wa kusimamishwa kwa "uwepo wa makampuni nchini Kenya hadi kuwe na mfumo wa kisheria wa udhibiti wa data za siri na watoa huduma pepe."

Kwa mujibu wa shirka la Reuters, Worldcoin, ilisema "haijaona chochote rasmi kilichotangazwa na Kamati hiyo moja kwa moja."

Ripoti ya jopo hilo itawasilishwa katika Bunge la Kitaifa ili kuzingatiwa na kupitishwa baadaye.

TRT Afrika na mashirika ya habari