Mapigano yameongezeka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo jeshi la taifa ilifukuzwa mwanzoni mwa mwaka. Haya ni kulingana na Umoja wa Mataifa.
Baada ya utulivu wa miezi sita, mapigano yalianza tena mwezi huu kati ya makundi yenye silaha na waasi wa M23 katika jimbo la Kivu Kaskazini, ilisema Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA).
Takriban raia 20 wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa tangu "kuzuka tena kwa mapigano makali" katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), OCHA ilisema.
"Zaidi ya watu 84,700 walikuwa wamelazimishwa kukimbia makaazi yao," OCHA ilisema, ikibainisha upatikanaji wa misaada "ulizuiliwa sana" kutokana na "kuongezeka kwa mapigano".
Kuongezeka kwa mapigano
Mapigano yapo katika maeneo ambapo jeshi la Afrika Mashariki la maelfu kadhaa lilitumwa mapema mwaka wa 2023, kwa nia ya kushika doria katika eneo ambapo kulikuwa na makundi yenye silaha.
Ripoti zaonyesha kuwa kwa muda, katika eneo la Kitshanga, mji wa kimkakati ulio kilomita 50 (maili 30) kutoka mji mkuu wa jimbo la Goma, hakujakuwa na vita kutokana na udhibiti wa kijeshi wa Afrika Mashariki.
Waasi wa M23, wanaoungwa mkono na Rwanda, wameteka maeneo ya Kivu Kaskazini, na kuwafanya zaidi ya watu milioni moja kuyahama makazi yao tangu kuibuka tena na kuanzisha mashambulizi mwishoni mwa 2021.
Makumi ya makundi yenye silaha yanafanya kazi mashariki mwa DRC, urithi wa vita vya kikanda ambavyo vilipamba moto katika miaka ya 1990 na 2000.