Shirika la World Meteorological Authority inaonya kuwa kuna ongezeko ya viwango vya joto duniani  / Picha: AP

Shirika la World Meteorological Authority inaonya kuwa kuna ongezeko ya viwango vya joto duniani na nchi za Afrika pia zimeathiriwa,

"Maeneo makubwa ya Afrika Kaskazini, bahari ya Mediterania, Asia na kusini mwa Marekani yamekumbwa na ongezeko ya joto sambamba ," shirika hilo limesema.

Barani Afrika Tunisia, Algeria na Sudan zimeripoti kiwango cha juu cha joto / Photo:AP 

Kwa mfano nchini Algeria wataalam wanasema hali joto katika mji mkuu wa Tunis zimefika nyuzi 49.

Baadhi ya maeneo nchini Tunisia yameripoti kiwango cha hali joto ya juu ya nyuzi 51.

"Joto kali linashika sehemu kubwa za Ulimwengu wa Kaskazini katika majira haya ya joto kali. Rekodi mpya za halijoto ya kila siku zimevunjwa na inawezekana kwamba rekodi zingine za kitaifa zinaweza kupitwa," WMO imesema

Lakini je, ukikumbwa na ongezeko la joto katika eneo unapoishi unafaa kufanya nini?

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom ametoa mapendekezo kadhaa dihi ya kujiokoa kutoka kwa mawimbi ya joto.

  • Vaa nguo nyepesi
  • Kunywa maji mengi
  • Punguza shughuli za nje wakati wa saa za kilele na epuka shughuli nyingi
  • Angalia wapendwa walio katika mazingira magumu, haswa wazee na watoto wachanga
  • Usiwaache watoto au wanyama wa nyumbani kwenye magari yenye joto
  • Jihadhari na dalili zinazohusina na joto

TRT Afrika