KNH imetoa muda wa siku 7 wahusika wachukue miili yao . /Picha: Wengine / Photo: AFP

Katika tangazo lililotolewa siku ya Jumanne, Novemba 26, hospitali ya Kenyatta ilitangaza kuwa kuna miili 262 ambayo haijachukuliwa. Likisema ya kwamba familia zina muda wa siku saba tangu tarehe ya tangazo hilo kuchukua miili ya wapendwa wao, vinginevyo itatupwa.

"Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta ina miili kadhaa ambayo haijachukuliwa katika nyumba yake ya hifadhi ya maiti. Kulingana na Sheria ya Afya ya Umma (Cap 243) Kanuni za Sheria ya Afya ya Umma [Hifadhi za Maiti za Umma], 1991).

"Kulingana na hospitali hiyo, miili mingi iliyoachwa ni ya watoto, huku hospitali ikiwa na miili 16 pekee ya watu wazima. "Wananchi wanaopenda kutambua na kuchukua miili hiyo wanaombwa kufanya hivyo ndani ya siku 7, la sivyo hospitali itatafuta idhini ya mahakama kutupa miili hiyo," tangazo hilo lilisema.

Hospitali hiyo imetangaza kuwa imepokea idhini ya kutupa miili saba. Ikiwa familia za miili mingine ambayo haijachukuliwa hazitajitokeza kuichukua, miili hiyo pia itatupwa.

Chini ya Sheria ya Afya ya Umma (Cap 242), hakuna mwili unaoruhusiwa kubaki katika hifadhi ya maiti kwa zaidi ya siku 10 bila kuchukuliwa. Ikiwa mwili haujachukuliwa ndani ya siku 21, mamlaka inahitajika kupata amri ya mahakama kwa ajili ya kuiupa, baada ya kutolewa kwa tangazo la umma la siku 14 kutafuta jamaa wa karibu wa maiti hiyo.

Kwa wale wahusika, orodha ya miili iliyoachwa inapatikana katika nyumba ya hifadhi ya maiti ya KNH Farewell Home na pia inapatikana kwenye tovuti ya taasisi hiyo.

Hii si mara ya kwanza kwa hospitali hiyo kutoa notisi kwa wenye maiti kuchukua miili yao.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT Afrika