Ethiopia inasema inataka kuungana na kundi la BRICS / Picha: AFP

Ethiopia inasema inataka kujiunga na muungano wa BRICS ambao unajumuisha Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini.

Msemaji wa serikali ya Ethiopia, Meles Alem ameambia waandishi wa habari kuwa serikali tayari imetoa ombi rasmi kwa kikundi hiki kujiunga nao.

"Tunatarajia BRICS itatupatia jibu chanya kwa ombi ambalo tumetoa," Alem alisema.

Brazil Urusi, India na China zilifanya mkutano wao wa kwanza mnamo 2009 nchini Urusi na Afrika Kusini ikajiunga mwaka 2010.

Nchi za BRICS zimekuwa injini kuu za ukuaji wa uchumi duniani kwa miaka mingi.

Kwa muda, nchi hizi zimekuwa zikikutana ili kujadili masuala muhimu chini ya mihimili mitatu ya kisiasa na usalama, kiuchumi na kifedha na kiutamaduni na kubadilishana watu na watu.

Meles amesema Ethiopia imekuwa mwanachama na mwanzilishi wa taasisi nyingi za kimataifa, na kuwa nchi hiyo itaendelea kufanya kazi na taasisi za kimataifa zinazoweza kulinda maslahi yake.

Ethiopia, nchi iliyo katika pembe ya Afrika inachukua nafasi ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, lakini kiuchumi iko nafasi ya 59 tu duniani kwa mujibu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF.

Hii ni chini ya nusu ya idadi ya watu wa Afrika Kusini ambayo ndiyo wanachama wenye idadi ya watu wachache zaidi katika BRICS.

Mwaka jana Argentina, nchi nafasi ya 23 kwa uchumi mkubwa duniani, ilisema iliungwa mkono rasmi wa China kujiunga na kundi hilo, ambalo linaonekana kuwa na nguvu kubwa katika soko linaloibukia badala ya soko la Magharibi.

Afrika Kusini ilisema Alhamisi itakuwa mwenyeji wa mkutano ujao wa marais wa BRICS, mwezi Agosti kama ilivyopangwa, huku kukiwa na uvumi kwamba unaweza kuhamishiwa mahali ambapo Rais wa Urusi Vladimir Putin hatalazimika kukamatwa kwa tuhuma za uhalifu wa kivita.

TRT Afrika