Kwa sasa sekta ya viwanda inachangia asilimia tano tu ya jumla ya ajira ya Ethiopia/ Picha: Wengine

Wizara ya viwanda ya Ethiopia imetangaza mpango wa kukidhi mahitaji yote ya kitaifa ya chakula, vinywaji na nguo kupitia utengenezaji wa bidhaa za ndani,katika miaka mitatu pekee.

Kwa sasa, uzalishaji wa ndani unachangia asili mia 38 ya mahitaji ya kitaifa, lakini mipango iko tayari kuongeza hii hadi asilimia 60 katika muongo ujao.

Sekta ya viwanda inachangia asilimia tano tu ya jumla ya ajira ya Ethiopia.

Mpango huo unalenga kupunguza gharama ya serikali ya kununua bidhaa hizo kutoka nje kwa takriban dola bilioni 2.3 kila mwaka.

Bidhaa 96 zimechaguliwa kuongoza jitihada hii ya kuelekea kujitegemea.

Ethiopia inakumbwa na changamoto ya kiuchumi iliyotokana na vita vilivyoendelea eneo la kaskazini mwa nchi hiyo kwa miaka miwili ( kati ya 2020 na 2022).

Maafa ya vita hivi ilifanya sekta ya viwanda nchini humo kupata pigo baada ya Marekani kuiondoa Ethiopia kutoka kwa nchi ambazo zinanuafika kutoka kwa Sheria ya Ukuaji na Fursa Afrika,AGOA.

Marufuku hiyo ilianza Januari 1, 2022, baada ya Marekani kushutumu Ethiopia kwa janga la kibinadamu huko Tigray na mikoa ya karibu.

Sera mpya ya utengenezaji bidhaa inalenga kuhuisha sekta hiyo na kuongeza mchango wake wa Pato la Taifa, ambalo limeonekana kupungua katika miaka ya hivi karibuni.

Ikiwa na thamani ya dola milioni 852.2 ya bidhaa zinazotengenezwa nchini tayari kuchukua nafasi ya uagizaji mwaka huu wa fedha, Ethiopia iko njiani kuchukua nafasi ya uagizaji wa thamani ya dola bilioni 2.3 na bidhaa za nyumbani.

TRT Afrika