Huku Ethiopia ikielekea kuifungua sekta yake ya mawasiliano benki kuu ya Ethiopia imetoa idhini ya huduma ya pesa kwa simu kutoka kwa Safaricom PLC, katika muungano wa makampuni manne.
Kampuni hii ya kigeni na mwekezaji wa kwanza wa kigeni katika sekta hiyo kupata leseni.
Nchi hiyo sasa itakuwa na huduma ya MPESA, huduma za pesa kwa njia ya simu ambazo zilifadhiliwa nchini Kenya na kampuni hiyo.
Mnamo Desemba mwaka jana, bunge la Ethiopia liliidhinisha mfumo wa malipo ulilorekebishwa, ambayo liliruhusu makampuni ya kigeni kushiriki katika shughuli za mfumo wa malipo.
"Hii itarahisisha ushiriki wao bila haja la kusubiri marekebisho ya sheria ya benki," Gavana wa Benki Kuu Mamo Mihretu alisema.
Ethiopia iliamua kufungua sekta yake ya mawasiliano mnamo Oktoba 2022 ilipotoa leseni kwa Safaricom PLC, na kumaliza ukiritimba katika sekta za mawasiliano nchini humo chini ya kampuni ya kitaifa ya Ethio Telecom.

Nchi bado ina mipango ya kutoa leseni kwa waendeshaji wengine wawili wa kigeni.