Kabla ya vita kuanza Novemba 2020 wanafunzi wapatao 124,000 walijiandikisha kufanya mtihani wa darasa la nane /Picha Prof. Kindeya Gebrehiwot

Wanafunzi katika eneo la Tigray nchini Ethiopia wanafanya mtihani wao wa kuhitimu elimu ya msingi kwa mara ya kwanza tangu vita vilipozuka katika eneo hio mwaka wa 2020.

Kuanza kwa mtihani huo Jumatano kunaonekana kama hatua muhimu, sio tu kwa watoto ambao elimu yao ilisimamishwa na vita vya tangu mwaka 2010 , pamoja na na janga la Uviko-19 kwa nchi kwa ujumla.

Kabla ya ghasia hizo, wanafunzi wapatao 124,000 walijiandikisha kufanya mtihani wa darasa la nane ili kumaliza shule yao ya msingi, Ofisi ya Elimu ya mkoa wa Tigray ilisema.

Lakini ni takriban nusu ya waliohitimu ambao wanafanya mtihani katika shule 1007 katika kanda hiyo.

Kupungua kwa idadi hiyo kunachangiwa na idadi kubwa ya watu waliohama makazi yao na kuendelea kufungwa kwa shule pamoja na ukosefu wa usalama katika baadhi ya maeneo, Mkurugenzi wa Wakala wa Tathmini na Mitihani ya Kielimu katika eneo hilo Kinfe Fisha aliliambia gazeti la Addis Standard.

Ofisi ya Elimu ya Mkoa ilikuwa imetangaza kufunguliwa tena kwa shule mwezi Mei kufuatia kurejea kwa amani.

Serikali ya Ethiopia ilitia saini mkataba wa amani na waasi wa Tigray People Liberation Front mwaka jana ili kumaliza mzozo wa miaka miwili ambao uliua maelfu ya watu na mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao.

Lakini Kiros Guesh, Mkuu wa Utawala wa Muda wa Ofisi ya Elimu huko Tigray, amesema kuwa kuwa shule 552 zimesalia ''zisizoweza kufikiwa'' kwa sababu hali ya usalama ilikuwa bado tete.

Aliwaambia waandishi wa habari wiki jana kuwa zaidi ya ''asili mia 77 ya watoto wa shule'' huko Tigray hawakuwa na shule.

Ni asilimia 23 tu ya wanafunzi milioni 2.4 wa eneo hilo walikuwa wamefaulu kurejea shuleni baada ya vita.

TRT Afrika