Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limezindua nembo mpya ya makala ya nne ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake, inayotarajiwa kuanza nchini Morocco, Novemba 9, 2024.
Katika taarifa yake iliyoitoa Novemba 6, CAF imesema kuwa nembo hiyo ni alama ya "ujasiri na ubora wa soka la wanawake" kwa bara la Afrika.
Nyongeza ya zawadi hiyo, kulingana na CAF ni kutoa motisha kwa soka la wanawake barani Afrika.
Michuano ya za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa wanawake inashirikisha timu nane zikiwemo Aigles de la Medina ya Senegal, EDO Queens kutoka Nigeria na University of the Western Cape ya Afrika Kusini.
Nyingine ni Tutankhamun ya Misri, CBE FC ya Ethiopia, Mameodi Sundowns kutoka Afrika Kusini, ASFAR ya Morocco na TP Mazembe kutoka DRC.
TRT Afrika