Bunge la Kitaifa la Kenya limepitisha mswada tata wa nyumba maarufu kama 'Affordable Housing 2023,' unaolenga kuipa serikali mwanga wa kuanza kutekeleza mpango wa rais wa makazi bila kukiuka sheria.
Mswada huo unaifungulia serikali uwezo wa kuanza tena kukusanya ushuru wa nyumba wa 1.5% kwa malipo ya jumla ya wafanyakazi. Hata hivyo, watu ambao hawajaajiriwa katika sekta za maalamu watalazimika kulipa ushuru huu.
Wabunge 141 walipiga kura kuunga mkono mswada huo dhidi ya 58 walioupinga.
Ikiwa maseneta watapiga kura kama wenzao wa Bunge la Kitaifa, ushuru huu ambao ulikuwa umetangazwa kuwa kinyume na katiba na mahakama, utaletwa upya.
Katika mkutano na wanahabari, viongozi wa upinzani walimshutumu Rais Ruto kwa kuwalazimisha wabunge kuupigia kura mswada huo licha ya kutopendwa kwake na wananchi.
Mswada huu ulirekebishwa kabla ya kurudishwa bungeni.
Chini ya mswada uliorekebishwa, wanunuzi wa nyumba za bei nafuu hawatahitajika kutoa asilimia 10 kwanza kabla ya ununuzi.
Wakenya walikuwa wamelalamika kuwa mahitaji hayo yangezuia idadi kubwa ya Wakenya kushiriki katika mpango huo.
Mahakama Kuu ilitoa maamuzi Novemba 28, 2023, kuhusu malalamiko ya kikatiba ambapo ilihitimisha kuwa Ushuru wa Nyumba Nafuu ikidai kuwa ulikiuka masharti ya Katiba kwa vile haukuwa na mfumo wa kisheria wa kina.