Rais wa Kenya William Ruto alisema serikali itachukulia hatua dhidi ya wapangaji, wafadhili, waongozaji, na washiriki wa vurugu na machafuko / Picha: AFP

Bunge la Kenya limepitisha ombi la serikali la kutaka vikosi vya jeshi kuchukua ulinzi wa usalama wa nchi.

Hii inafuatia uamuzi wa Rais William Ruto wa Juni 25, 2024, katika hotuba yake kwa nchi baada ya baadhi ya waandamanaji kuvamia bunge na majengo mengine ya serikali.

Katika hotuba hiyo Jumanne usiku, Ruto alisema serikali itachukulia hatua dhidi ya wapangaji, wafadhili, waongozaji, na washiriki wa vurugu na machafuko.

Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetangula amelaani vikali kuingiliwa kwa majengo ya bunge/ picha: AFP

Spika wa Bunge Kenya amekashifu kuvamiwa kwa majengo ya bunge na majengo mengine ya taifa. Tarehe 25 Juni 2024 waandamanaji ambao walikuwa wanapinga muswada wa fedha 20204 walivamia majengo hayo na kusababisha uharibu wa mali.

"Baraza hili linakubali ombi la Baraza la Ulinzi la Kenya la tarehe 26 Juni 2024 na kwa maslahi ya usalama wa taifa limeidhinisha kutumwa kwa Jeshi la Ulinzi la Kenya, KDF ili kuunga mkono Huduma ya Kitaifa ya Polisi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Kenya yaliyoathiriwa na maandamano ya vurugu yanayoendelea ambayo yamesababisha uharibifu kwa miundombinu muhimu hadi usalama urejeshwe," imesema taarifa ya Bunge.

Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetangula amelaani vikali kuingiliwa kwa majengo ya bunge.

Majengo ya bunge kwa sasa yako chini ya ulinzi mkubwa /Picha: AFP 

"Mimi si mgeni katika mazungumzo ambayo yamekuwa yakiendelea hapa nchini kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha na hali ya uchumi wa Taifa kwa ujumla, nawapongeza vijana wa taifa hili kwa kuongoza katika mjadala huu na Fursa ya kuwa hai katika wakati kama huu kuona watoto wetu wakishiriki na kuunda mwenendo wa taifa letu," Spika wa Bunge ya Kenya Moses Wetangula amesema.

Majengo ya bunge kwa sasa yako chini ya ulinzi mkubwa huku maafisa wa polisi wengi wakionekana kushika doria nje na ndani ya majengo ya bunge.

"Ni muhimu kwamba mijadala hii ifanyike kwa mpangilio na maana, ndani ya mipaka ya sheria ili yapate matokeo yanayotarajiwa. Vurugu, ukosefu wa heshima na uharibifu wa mali na mashambulizi ya wazi dhidi ya taasisi za umma havitakubaliwa," Spika ameongezea.

TRT Afrika