Amri hiyo ilisisitiza dhamira ya Türkiye ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na uharamia wa baharini na wizi wa kutumia silaha /Picha: AA

Bunge la Uturuki limeongeza muda wa vikosi vya jeshi la wanamaji la Uturuki katika Ghuba ya Aden, maji ya eneo la Somalia, Bahari ya Arabia na maeneo ya jirani kwa mwaka mwingine.

Amri ya rais iliyopitishwa na bunge la nchi hiyo siku ya Jumatano ilisisitiza jinsi maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yalivyochukuliwa dhidi ya uharamia na wizi wa kutumia silaha katika maeneo hayo kuanzia 2008 hadi 2021.

"Kwa kupeleka wanajeshi wa jeshi la wanamaji wa Kikosi cha Wanajeshi wa Uturuki, hatua madhubuti zimechukuliwa ili kuhakikisha usalama wa meli za kibiashara zenye bendera ya Uturuki na zinazosafiri katika eneo hilo," ilisema amri hiyo.

"Kushiriki kikamilifu kumefanywa katika operesheni za pamoja dhidi ya uharamia wa baharini, ujambazi wa kutumia silaha na ugaidi baharini, zinazoendeshwa na jumuiya ya kimataifa," iliongeza.

Amri hiyo pia ilisisitiza dhamira ya Uturuki ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na uharamia wa baharini na wizi wa kutumia silaha.

Ilisema kuwa Uturuki imekuwa ikiunga mkono juhudi katika hili na imeshiriki kikamilifu katika mipango ndani ya UN, NATO, EU, na Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO).

TRT Afrika