Chombo cha mbao kilikuwa kimesheheni ndizi. Picha / Faili / Reuters

Watu 14 hawajulikani walipo baada ya mashua kupinduka kwenye ziwa kusini mwa Ethiopia, maafisa wa eneo hilo walisema Ijumaa.

Boti hilo , lililokuwa limesheheni ndizi, lilizama siku ya Alhamisi katika Ziwa Chamo, kusini mwa mji mkuu Addis Ababa, ofisi ya mawasiliano ya eneo la Gamo ilisema.

Ziwa Chamo katika Bonde Kuu la Ufa, ambalo lina kina cha mita 14, ni makazi ya mamba na viboko.

Waokoaji waliwapata manusura wawili ambao walifaulu kusalia kwa kushikilia madumu, maafisa hao walisema, na kuongeza kuwa msako unaendelea kuwatafuta abiria wengine.

Wafanyakazi 15 ambao kazi yao ilikuwa ni kupakua ndizi na mwendeshaji mizigo walikuwa ndani ya chombo hicho, kamanda wa polisi wa eneo hilo Reta Tekla alisema.

Haikuweza kufahamika mara moja kwa nini ilizama.

TRT Afrika