Uturuki imekuwa ikiishinikiza Marekani kusimamisha mapigano mara moja na ya kudumu huko Gaza huku Marekani ikisisitiza kuunga mkono haki ya Israel ya "kujilinda" yenyewe. / Picha: AA 

Huku eneo la Mashariki ya Kati likikabiliwa na mgogoro na masuala kadhaa muhimu kati ya nchi zao mbili , Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na waziri wa mambo ya nje Hakan Fidan wamekutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken juu ya masuala yanayowakabili ikiwemo vita vya Israel dhidi ya Gaza inayozingirwa na Israel, hatua za mwisho za kukamilisha uidhinishaji wa Uturuki.

Maswala waliyokuwa nayo ni pamoja na ombi ya NATO ya Sweden, na idhini ya bunge la Marekani kwa uuzaji wa ndege za kivita za F-16 kwa Uturuki.

Mkutano wa Jumamosi katika Jumba la Vahdettin huko Istanbul ulijumuisha mkuu wa Shirika la Kitaifa la Ujasusi la Uturuki (MIT) Ibrahim Kalin na balozi wa Marekani huko Ankara Jeffry Flake.

Hakuna habari zaidi iliyotolewa kuhusu mkutano huo wa faraga,

Mapema siku hiyo, Blinken na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan walikuwa wamekutana ana kwa ana.

"Katika mkutano huo, Mawaziri walijadili vita na mgogoro wa kibinadamu huko Gaza, mchakato wa Sweden kujiunga na NATO, masuala ya nchi hizo mbili na kikanda," Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilisema kwenye X.

Fidan na Blinken wamepigiana simu na kufanya mikutano kadhaa tangu Oktoba 7 kujadili Gaza, miongoni mwa masuala mengine ya nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na Sweden kujiunga na NATO na Marekani kufanya mauzo ya ndege za kivita za F-16 kwa Ututuki.

Wakati wa ziara yake ya kikanda, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Blinken atasisitiza kulinda maisha ya raia, kuwaachilia mateka, kupeleka misaada ya kibinadamu Gaza, kurejesha huduma muhimu, na kuzuia kulazimishwa kwa Wapalestina kutoka Gaza.

Pia atashughulikia hatua za haraka za kupunguza ghasia, maswala ya utulivu, na kupunguza mivutano, ikiwa ni pamoja na kuzuia mashambulizi ya Houthi nchini Yemen na kuepuka kuongezekakwa vurugu nchini Lebanon.

Blinken atathibitisha dhamira ya Marekani ya kufanya kazi na washirika kwa ajili ya amani ya mashariki ya kati, akisisitiza maswala ya taifa la Palestina pamoja na Israel, ilisema idara hiyo.

Ziara yake inakuja huku kukiwa na ongezeko la maafa ya kibinadamu huko Gaza kutokana na mashambulizi yote mawili ya Israel na kuzingirwa kwake.

TRT Afrika