Benki ya Maendeleo la Afrika , AFDB, inasema kuwa Afrika ina uwezo ya kumaliza njaa : Picha Getty / Photo: Getty Images

Sehemu tofauti za bara la Afrika zinakumbwa na janga la njaa.

Katika kanda ya Afrika Mashariki pekee, sehemu za Kenya, Somalia, na Ethiopia zinakumbwa na athari ya tabianchi ambayo imepelekea misimu sita ya ukame.

Zaidi ya watu milioni 47 katika nchi hizi na zingine katika pembe ya Afrika wanalazimika kutegemea chakula cha msaada.

Benki ya Maendeleo la Afrika , AFDB, inasema kuwa Afrika ina uwezo ya kumaliza njaa kwa kuchukua hatua ikiwemo ufadhili thabiti.

"Lazima tuunganishe pamoja sayansi bora zaidi, teknolojia na ubunifu ili kuendesha mfumo wa kilimo wenye mafanikio ," Akiwunmi Adesina, rais wa benki ya AFDB aliuambia mkutano wa nane wa wiki ya biashara ya kilimo na sayansi barani Afrika ambao unafanyika jijini Durban, nchini Afrika Kusini.

Adesina alisema mifumo ya chakula ya Afrika ina uwezo wa kutoa thamani ya dola trilioni moja katika miaka saba ijayo.

Kamishna wa Umoja wa Afrika wa Uchumi wa kilimo cha vijijini balozi Josefa Leonel Correia Sacko ulimwengu uko katikati ya janga la njaa linalosababishwa na sababu zinazoendelea, pamoja na athari ya Uviko-19 na mabadiliko ya hali ya hewa.

"Afrika inahitaji kuongeza uwezo wake, ikiwa ni pamoja na sayansi, na kuwa makini badala ya kukabiliana na mishtuko, " Sacko alisema.

Aliongezea kuwa bara linafaa kuchukua fursa ya idadi ya vijana wake na mtaji mkubwa wa asili.

"Hebu tufungue uwezo tulionao… tunapaswa kulisha waafrika na tunapaswa kulisha dunia," Sacko alisema.

Wiki ya biashara ya kilimo na sayansi barani Afrika huleta pamoja wadau 1,500 kila baada ya miaka mitatu kama jukwaa kuu la bara la wadau wa kilimo na utafiti wa biashara ya kilimo na uvumbuzi barani Afrika.

TRT Afrika